WAZIRI MKUU CASSIM MAJALIWA AFUNGUA CHANELI YA UTALII

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli mpya ya utalii inatarajiwa kuvutia watalii wengi zaidi kuja nchini sambamba na kuongeza pato la taifa. Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipokuwa akizindua chaneli hiyo ya utalii inayojulikana kama āTanzania Safari channelā Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli hiyo mpya itatoa fursa ya kutangaza wanyama mbalimbali waliopo katika hifadhi za wanyama, utamaduni wa watanzania pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kuvutia watu wengi zaidi kuja kufanya utalii na hatimaye kuongeza kiasi cha fedha kitachochangia katika pato la taifa. āChaneli hii ni njia muhimu ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi yetu, ambapo itaongeza idadi ya watu watakaotembelea Tanzaniaā alisema Waziri Mkuu Majaliwa Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa kwa sasa watalii wanaokuja nchini kwa mwaka ni milioni 1.3 , na matarajio ya Serikali ni kuon...