RAIS TRUMP APOKEA BARUA KUTOKA KOREA KASKAZINI

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anatarajia kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwa mara ya pili katika hatua ya Washington kuendelea kutafuta mbinu za kuifanya Korea Kaskazini kuachana kabisa na silaha za nyuklia. Trump amesema hivi karibuni alipokea barua "nzuri" kutoka kwa Kim Jong-un, akidai kuwa Marekani imepiga hatua kubwa katika mazungumzo na Pyongyang bila ya kueleza maudhui ya barua hiyo. "Tulianzisha uhusiano mzuri sana, mambo mazuri yanayotokea," Trump aliwaambia waandishi wa habari katika White House. "Tulifanya mkutano na Kim miezi sita iliyopita huko Singapore. Tunaweza kuwa na mkutano mwingine.Ningependa kukutana na vilevile yeye anataka kukutana." Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya hotuba ya kitaifa ya KimJong Un siku ya Jumanne ambapo alisema kuwa atakuwa tayari kufanya mkutano tena na Trump. Hata hivyo Kim Jong Un ameonya kuwa Pyongyang inaweza kufuata "njia mpya" ikiwa Washington haitoon...