Posts

Showing posts from January 31, 2019

HARMONIZE KUKAMATWA NA POLISI KISA BANGI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema ameongea na Gavana wa Ghana kumchunguza msanii, Harmonize ambaye yupo nchini humo kama anatumia bangi ili kama ni kweli akirudi amuweke rumande.  Hatua hiyo imekuja baada ya Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.  "Nimemuona mtu mmoja yuko Ghana kule ule moshi unavyotoka ni kama wa Bangi na tayari nimeshaongea na rafiki angu Gavana wa Ghana pale wanisaidie kumfuatilia Harmonize anatumia Bangi au sigara na kama anatumia bangi akitua hapa ni Lock Up moja kwa moja namna unavyojithaminisha ndivyo serikali itakavyo kuthamini," alisema Makonda.  Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019  wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. 

BILLNAS KUJA NA COLLABO NA ALIKIBA

Image
Msanii wa Muziki, Bill Nas amefunguka kuhusu ujio wa kolabo yake na AliKiba.  Bill Nass akiongea katika kipindi cha The PlayList cha Times FM amesema kuwa kolabo na msanii huyo tayari wameshafanya.  "Kolabo na Alikiba ipo na tayari tumeshafanya bado kutoka kwasababu ya taratibu zao kwasababu Ali yuko chini ya Sony hata kutoa ngoma pia kuna utaratibu wake, nasubiri tu utaratibu wao kama itatoka mwakani au mwaka huu," alisema Bil Nass.  Billnass kwasasa anatamba na kibao cha wimbo wake mpya unaoitwa 'Funga Geti' aliomshirikisha Roma ambao mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube una 366,181 views.