Posts

Showing posts from October 8, 2019

Wema sepetu ataja sehemu atakayozikwa akifariki

Image
KWELI mambo ni mengi muda mchache! Staa wa Bongo Movies asiyechuja, Wema Isaac Sepetu amekumbushia kuwa sehemu atakayozikwa ni palepale pembeni ya baba yake, Balozi Sepetu kule Chuini visiwani Zanzibar.   Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema amesema ni muhimu kukumbusha watu kila mara maana wanaweza kupitiwa na kumpeleka sehemu ambayo mtu haipendi.   ā€œNajua watu wanaweza kujisahau hivyo ni vizuri kuwakumbusha mahali ambapo mtu anataka apumzishwe siku ikiwadia,ā€ amesema Wema

Mo Sallah yuko tayari kucheza dhidi ya Manchester united

Image
Mshambuliaji kutoka nchini Misri na klabu ya Liverpool Mohamed Salah, ana matumaini makubwa ya kuwakabili Manchester United, kufuatia taarifa za jeraha lake kuleta ahuweni kwa mashabiki.   Salah aliumia jumamosi, wakati wa mchezo dhidi ya Leicester City, baada ya kuchezewa rafu na kiungo Hamza Choudhury, kitu ambacho kiliwashtua mashabiki wa Liverpool ambao wanahitaji kumuona akiendelea kuzichachafya ngome za timu pinzani msimu huu.   Majibu ya vipimo alivyofanyiwa mshambuliaji huyo, yameeleza kuwa hakuumia sana kama ilivyofikiriwa, na kwamba aliteguka kifundo cha mguu kwa kiasi kidogo.   Hata hivyo mpaka sasa haijatangazwa ni lini Salah atarejea uwanjani, ila kinachoelezwa ni kwamba hatakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Manchester United.   Choudhury alionyeshwa kadi ya njano kutokana na rafu aliyomchezea Salah, huku meneja wa Liverpool Jurgen Klopp akiamini kwamba lilikuwa ni tukio ambalo lilipaswa mchezaji huy...

Justin Bieber atangaza siku ya kuachia Album mpya

Image
MWANAMUZIKI kutoka pande za Marekani Justine Bieber amewadokeza mashabiki zake ujio wa album yake mpya kabla ya mwaka huu kuisha.   Justine  Bieber ambaye hajatoa kazi yoyote tangu mwaka 2015 kupitia ukurasa wake wa instagram alipost video fupi akiwa na mke wake Hailey wakisema ā€œAlbum coming out this year. Another song coming out  soon.ā€