Posts

Showing posts from September 20, 2019

Golikipa wa chelsea amshambulia vikali De gea

Image
Kipa wa zamani wa Chelsea,  Mark Schwarzer, amesema kuwa mlinda mlango namba moja wa Manchester United, David de Gea amekuwa akionyesha uwezo wa kawaida tofauti na zamani.   Schwarzer amesema kuwa mabao mengi anayofungwa yanatokana na makosa yake binafsi.   ā€œMabao mengi anayofungwa yametokana na makosa yake binafsi, makosa aliyofanya kipindi hicho ni mengi kuliko aliyofanya miaka sita au saba, iliyopita,ā€ alisema Schwarzer .   Schwarzer amesema De Gea alikubali kufungwa kwa uzembe kwenye michezo ya Ligi Kuu England wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace na Southampton.   De Gea ambaye amesaini mkataba mpya ndani ya United utakaodumu mpaka 2023, amekuwa akibebeshwa lawama kwa kufanya makosa yanayopelekea timu yake kufungwa.   Hivi karibuni mlinda mlango huyo mashuhuri wa mashetani wekundu alisaini mkataba mpya ambao unamuwezesha kubaki Old Trafford hadi mwaka 2023 huku akilipwa mshahara wa Paundi 500,000 kwa juma.

Mrembo Hamisa Mobetto atamani maisha ya ndoa

Image
Hamisa Mobeto siku za nyuma aliwahi kusema Hana mpango wa kuolewa na kijana wa kitanzania Bali mipango yake ni kuolewa na mzungu   Awali alisema yeye anataka labda mwanaume mzungu au mtu mzima, awe alishawahi kuachwa au mgane kwa hiyo ndio hivyo, na kusema kijana kwake hapana.   Hamisa Anataka mtu wa kumuoa awe angalau miaka 45 kwa sababu yeye mwenyewe ana watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wake