NJIA ZA KUONGEZA DAMU MWILINI MWAKO

Anemia hali inayotokea pale kiasi cha seli nyekundu za damu zinapokuwa chache kuliko kawaida au seli hizi nyekundu zinapungukiwa na chembechembe za hemoglobin. kwa lugha rahisi tunasema ni upungufu wa damu mwilini. Kuishiwa damu hupelekea mwili kuwa mchovu muda mwingi, misuli kuishiwa nguvu, mood kubadilika na kupata ganzi mara kwa mara. Tatizo linavokuwa kubwa zaidi linaweza kupelekea matatizo kwenye moyo, ubongo na viungo vingine vya mwili. Hivyo ili kuepukana na kupatwa na upungufu wa damu mwilini zifutazo ni hatua za kuongeza damu mwilini: Kuimarisha ufanyaji kazi wa Bandama&t;/b> Bandama ni kiungo kinachohusika na utengenezwaji wa seli nyekundu za damu na pia kuweka msawazo wa majimaji mwilini. kama bandama yako ina shida basi hii ni sababu ya kwanza kwanini una upungufu wa damu mwilini. Tumia vyakula vifuatavyo ili kuweka sawa bandama yako.vyakula kama spinach na mboga zingine za kijani, maboga na mbegu za maboga na karanga. kuimarisha mfumo wa chaku...