Posts

Showing posts from December 13, 2018

ABDI BANDA AFUNGUKA KUONDOKA BAROKA FC YA S.A

Image
Kwa mujibu wa Magazeti ya Afrika Kusini, beki Mtanzania,anayeichezea Baroka FC Abdi Banda ataondoka kwenye klabu hiyo muda wowote kuanzia Krismasi.  Habari za uhakika kutoka ndani ya Baroka ni kwamba Banda mwezi huu atajiunga na klabu moja iliyoko kwenye Jimbo la Gauteng Kaskazini mwa Afrika Kusini ambapo Spoti Xtra limebaini kwamba ni Kaizer Chiefs.  Habari zinasema kwamba mazungumzo bado yanaendelea baina ya klabu hizo lakini tayari Baroka wameshanunua mbadala wa Banda ingawa yeye hajui lolote.  Banda akiwa na mke wake dada wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ā€˜Alikiba’, Zabibu Kiba.  Banda alijiunga na Baroka ambayo haifanyi vizuri kwenye Ligi ya Afrika Kusini, mwaka jana akitokea Simba.  Amecheza mechi kadhaa kwenye klabu hiyo huku akisumbuliwa na majeraha, uongozi umesisitiza kwamba hauna mpango wa kubadilisha benchi la ufundi.  Mmoja wa viongozi wa Baroka amesema kwamba tayari wamemsajili Vusi Sibiya raia wa Afrika Kusini, mwezi uliopita kutoka...

MATUNDA YANAYOWEZA KUTUNZA NA KUIMARISHA NGOZI YAKO

Image
Wakati mwingine ili uweze kuboresha mwonekanao wa ngozi yako si lazima utumie makemikali yenye viambatano vyenye sumu ili uweze kufanya hivyo, bali inahitajika uweze kutumia matunda ambayo yana msada mkuubwa wa kuweza kufanya ngozi yako ing`are.   1.   Parachichi.   Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juisi lakini huenda watu  hawalipendi kwa sababu kwa kutokuwa na sukari katika radha yake. Tunda hili lina vitamin kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini kwa wale walitumialo mara kwa mara, wanashauriwa kula au kunywa juisi ya parachichi wakati wowote endapo kama huna matatazo yeyote yananahusiana na kuzidi kwa mafauta mwilini. Pia tunda hili huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara.   2.   Apple.   Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupema umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamin na madini kibao, pia lina kazi sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngoz...

MAGAZETI YA LEO 14/12/2018

Image

RAIS MSTAAFU WA GAMBIA "YAHYA JAMEH" AZUIWA KUINGIA MAREKANI

Image
Marekani imempiga marufuku Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh kuingia nchini humo kutokana na historia mbaya ya utawala wake iliyohusisha vitendo vya rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.  Uamuzi huo umetolewa Disemba 10 ikiwa ni miaka miwili tangu Jammeh alipolazimishwa kukimbilia uhamishoni nchini Equatorial Guinea. Aliondolewa kwa nguvu madarakani na Jeshi la Umoja wa Afrika baada ya kukataa kuachia madaraka kufuatia kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Adama Barrow.  Marekani imeeleza kuwa Jammeh amezuiwa kuingia nchini humo pamoja na familia yake yote, na kwamba uamuzi huo unatokana na sheria za nchi hiyo kwa maafisa wa Serikali za nchi nyingine ambao wanaaminika kujihusisha na vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa haki za binadamu.  Kwa mujibu wa Serikai ya Gambia inayoongozwa na Barrow, Jammeh aliiba zaidi ya $50 milioni za umma alipokuwa madarakani.  Kwa mujibu wa ripoti, Jammeh anamiliki majumba katika eneo la Potomac, Maryland nchini Marekani, Kilometa 2...

ALIKIBA AFUNGUKA KUHUSU MKATABA NA TIMU YAKE YA COASTAL UNION

Image
Mchezaji wa Timu ya Coastal Union na Msanii wa Muziki, AliKiba amefunguka kuhusu mkataba wake na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.  "Mkataba wa Coastal na mimi, Mimi silipwi siichezei kwa pesa nacheza for fun, napenda mpira na vile vile nineweza kutangaza coast, kutangaza zaidi na vilevile Caostal wanatangaza Mo fire , vilevile kuna vitu ambavyo tunasaidiana sisi kama kuendeleza timu ya Coastal iweze kuendelea kufika mbali siwezi kuanika kila kitu mzee baba  Alikiba amesema yupo mbioni kuanza kuuza jezi  za Coastal Union zenye namba yake (7) na zitakuwa na saini yake pia

THERESSA MAY ANUSURIKA KUTOLEWA MADARAKANI NA CHAMA CHAKE

Image
Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May amepata ushindi baada ya wanachama wa chama cha Conservative kupiga kura ya kutokuwa na imani na uongozi wake.  May ameungwa mkono na wabunge 200 katika kura hiyo huku wengine 117 wakiwa wamepiga kutokuwa na imani naye.  Waziri Mkuu huyo wa Uingereza atanusurika kupigiwa tena kura kama hiyo mpaka baada ya mwaka mmoja.  Chama cha upinzani kinaweza kuamua kupiga kura dhidi ya uongozi wa serikali ya May lakini wanachama wameamua kuwa huu sio muda  mwafaka.  "Matokeo ya kura ya leo yameonyesha kuwa wabunge hawana imani",alisema mwenyekiti wa kamati ya 1922,uongozi wa chama cha Conservative.  Brandy alipokea barua 48 za kutaka kura ya kutokuwa na imani ipigwe.  Hata hivyo waziri May amesema kuwa hana haja na kugombea katika uchaguzi mwaka 2022 na kwamba dhumuni lake kuu ni kuhakikisha anamalizana na suala zima la Brexit.

HARUNA MOSHI BOBANI ASAINI MKATABA YANGA

Image
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya African Lyon, Haruna Moshi ā€˜Boban’ sasa rasmi kuwa mali ya Yanga na kinachosubiriwa ni kuanza kazi tu na wakali hao wa Jangwani. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, Boban kutoka African Lyon amekubaliana na Yanga kuingia mkataba wa miezi sita.  Sasa ataanza kazi mara moja ili kuongeza nguvu katika kikosi cha Yanga ambacho kinaongoza Ligi Kuu Bara.  Boban amewahi kuichezea Simba kwa mafanikio makubwa. Alijiunga nayo mwishoni mwaka mwaka 2003 akitokea Coastal Union ambayo baadaye alirejea tena na kuichezea.

KUKOSA KITAMBULISHO CHA TAIFA NI KOSA KISHERIA - WAZIRI KANGI LUGOLA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wananchi wenye sifa ya kupata Vitambulisho vya Taifa nchini waende kujisajili katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho hivyo (NIDA) zilizopo katika Wilaya wanazoishi kwakuwa ni lazima kila Mtanzania awe nacho.  Akizungumza na wananchi wa Mji wa Kibara, Jimbo la Mwibara, Bunda, Mkoani Mara, Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alisisitiza kuwa ni lazima kila mwananchi raia wa Tanzania awe na kitambulisho cha Taifa.  ā€œVitambulisho hivi ni muhimu kuwa navyo, nawaomba Watanzania msipuuze hili zoezi, na pia napenda kusisitiza kwa mara nyingine muelewe vizuri kuwa vitambulisho hivyo vitatolewa kwa watanzania wenye sifa tu ambao watapita katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wasio raia,ā€ alisema Lugola.  Aidha Lugola alisema wapo wananchi ambao hawakujitokeza wakati usajili ulipokua unafanyika katika mitaa na vijiji vyao, na pia wapo ambao kipindi hicho walikua na miaka 17 na kukosa sifa ya kujisali, lakini kwasasa ...

FAHAMU MADHARA YA KUCHORA TATOO MWILINI

Image
Tattoo ni nini?   hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..   kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani.   hivyo kabla hujaamua kujichora tattoo basi madhara yake haya hapa..   Kansa ya ngozi;    hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.   Allergy ya ngozi;    haij...

VANESSA MDEE AFUNGUKA KUACHA NA JUX

Image
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee 'Vee Money' amefunguka juu ya madai yanayosambaa mitandaoni kuwa amemwagana na mpenzi wake, Juma Jux.  Vanessa ambaye yupo nje ya nchi kikazi amesema kuwa, hajamwagana na mpenzi wake huyo bali ni masuala ya kazi tu ndio yamewaweka mbali na kwamba hakuna kingine zaidi ya hicho.  Akizungumzia madai ya kuwa amemsaliti, Vanessa amesema kuwa hana tatizo kabisa na Jux ila kazi ndiyo zinazowafanya wasiwe karibu hivyo ndiyo maana watu wanawaona kama hawapo sawa.  ā€œMimi na Jux hatuwezi kuwa pamoja kila siku kuna kipindi kazi zinabana sana na ndio maana watu wanaona tumemwagana, niwatoe hofu tu mashabiki zangu kwamba tupo sawa na hakuna kitu chochote kibayaā€, amesema Vanessa.  Www.eatv.tv, imemtafuta Juma Jux ili kuzungumzia tuhuma hizo zilizoenea mitandaoni kuhusu kusalitiwa na mpenzi wake huyo lakini simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa.

WAGOMBEA UONGOZI 28 KUFUTWA UANACHAMA YANGA

Image
Jumla ya wanachama 28 wanaogombea nafasi za uongozi wa Klabu ya Yanga, wanatarajiwa kufutwa uanachama kutokana na kosa la usaliti la kwenda kuchukua fomu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).  Wagombea hao waliojitosa kuwania nafasi ya uongozi ni ile ya Mwenyekiti, Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Igangula na Erick Ninga.  Nafasi ya umakamu mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Yono Kevela wakati wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.  Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geofrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Faustin Peter Bisangwa.  Maamuzi hayo ya kuwaondoa uanachama wagombea hao yalitolewa jana kwenye kikao cha viongozi wa matawi ya kanda tano waliokutana juzi Jumatatu kwenye Makao Makuu ya kla...

PAPA FRANCIS WA KANISA KATOLIKI AWASHUSHA VYEO MAKADINALI WAWILI

Image
Papa Francis amewashusha vyeo makadinali wawili kufuatia kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yao huku mmoja akistafu na hivyo kufanya idadi ya makadinali watatu watakao kosekana kwenye baraza lake linalomshauri.  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi ya Waandishi Vatican, Mkurugenzi Greg Burke amesema kuwa kwa mujibu wa mkutano uliyofanyika tarehe 27, umeadhimia kadinali George Pell kutoka nchini Australia na mwenzake, Francisco Javier Errazuriz wa Chile kutoendelea kuhudumu kwenye baraza la hilo linalomshauri papa Francis kufuatia tuhuma zinazowakabili.  ā€œMnamo mwezi Oktoba, Papa aliwaandikia barua makadinali hao watatu wa kubwa, Kardinali Pell kutoka Australia, Kardinali Errazuriz kutoka Chile na Kardinali Monsengwo wa Kongo akiwashukuru kwa kazi yao,ā€ amesema Mkurugenzi huyo Burke na kuongeza kuwa hawatakuwa tena sehemu ya Baraza na wala Papa hakuwa na majina ya watu watakao chukua nafasi hizo.  Wawili hao hawakuwepo kwenye mkutano wa mw...

SHEIKH ALIETEKWA NA WATU WASIOJULIKANA ATAFUTWA NA POLISI

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna ameeleza juu ya tukio la kupotea kwa Mkuu wa Chuo Mkuu wa chuo cha Nyakato Islamic Institute kilichopo chini ya Taasisi ya Elimu ya The Registered Trustees of Islamic, Sheikh Bashir Gora na kudai jeshi linaendelea kumtafuta.  Akizungumza na www.eatv.tv Kamanda Shanna amesema ni kweli wamepokea taarifa za kupotea kwa Sheikh huyo hivyo ameagiza kufungwa kwa mipaka yote ya Mkoa wa Mwanza ili kuhakikisha kiongozi huyo anapatikana mapema iwezekanavyo.  Shanna amesema "ni kweli tumezipata taarifa za kupotea kwake, lakini unajua mtu akipotea huwezi kujua tatizo ni nini, na hatujui kwanini hapatikani na tumemtafuta kila mahali hapatikani, tumeshafunga mitambo yetu kwenye maeneo yetu yote."  Akizungumza hivi karibuni, Katibu wa Bodi wa taasisi hiyo, Sadik Mchola amesema tukio hilo lilitokea Disemba 6 chuoni hapo ambapo alikuja kijana mmoja kuulizia nafasi za kujiunga na chuo kwaajili ya mdogo wake.  ā€œKijana huyo alitukuta o...

WASANII WANAOWANIA TUZO ZA SOUNDCITY MVP AWARDS

Image
Majina ya wasanii ambao watawania tuzo ya SoundCity MVP Awards 2018 yametangazwa jana katika Website ya www.soundcitymvp.com na huku yakiwemo majina ya Wasanii wakubwa Kwenye muziki barani Africa na Kukiwa na mchuano mkali Kutokana na aina ya kazi ambazo wamekuwa wakizifanya kwa mwaka Huu wote  Katika List hiyo Majina Mbalimbali yametajwa na Wasanii Kutoka Tanzania Wamepenya Kwa Asilimia Kubwa … Wasanii Kama vanessamdee ,mbosso ,harmonize_tz ,mauasama ,navykenzoofficial na diamondplatnumz  Tuzo Hizi zitatolewa tarehe 05 Mwezi wa Kwanza 2019 Katika Ukumbi wa EKO Convention Centre Huko Nchini Nigeria .  NA HIZI NI BAADHI YA CATEGORY AMBAZO MAJINA YA WATANZANIA WANAOWANIA TUZO HIZI WAMETAJWA : šŸ‘‡  BEST MALE MVP  :  Nasty C  Cassper Nyovest  Davido  Wizkid  Burna Boy  #DiamondPlatnumz  Mr. Eazi  Olamide  AKA  #Harmonize  Shatta Wale  BEST FEMALE MVP:   Busiswa  Simi  Niniola  Tiwa ...