Posts

Showing posts from September 13, 2019

Jurgen Klopp achaguliwa kocha bora wa mwezi na Pukki mchezaji bora

Image
Meneja wa klabu ya liverpool ya jijini London ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa nane baada ya kuwapiga chini makocha wa Totenham,Manchester united na Manchester city, Timu ya liverpool imecheza michezo minne na kushinda mechi zote 4. Upande mwingine mshambuliaji wa klabu ya Norwich city Teemu pukki ameahindi tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nane baada ya kucheza mechi  4 na kufanikiwa kufunga magoli 5 katika michezo hiyo.

Kikosi cha Simba leo dhidi ya Mtibwa sugar

Image
Klabu ya Simba imetoa kikosi kitakachocheza leo dhidi Mtibwa sugar, kikosi hicho kina wachezaji 11 na 7 wa akibaki kikiwa kinaongozwa na Nahodha  Mohammed hussein, Mchezo huo utachezwa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Ben pol apigia msumari ndoa yake na Anerlisa

Image
Baada ya uvumi wa maneno ya waja kuhusu mastaa kuchumbia au kuchumbiwa na kuacha au kuachwa solemba, mwanamuziki wa RnB Bongo, Benard Paul ā€˜Ben Pol’ amevunja ukimya.  Baada ya kumchumbia mrembo tajiri kutoka nchini Kenya, Anerlisa Muigai, wengi walitarajia kuwa kilichokuwa kinafuata ni ndoa kati ya Ben Pol na mrembo huyo, lakini miezi ikawa inakatika tu huku baadhi ya wananzengo wakidai uchumba huo umevunjika.   Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, mapema wiki hii, Ben Pol alieleza kuwa mipango ya ndoa iko palepale. Alisema suala hilo ni la kifamilia zaidi hivyo mashabiki wake wasisikilize maneno ya watu, bali wasubiri waone nini kitakachofuata.   ā€œUnajua kuna kitu watu wanachanganya, mambo ya ndoa ni ya familia zaidi, siyo kila kitu unatakiwa kukiweka wazi. ā€œKwa hiyo, watu watulie ili waone nini kitatokea na kama ikitokea, muda ukifika wataona tu kwa sababu ndoa siyo jambo la siri na lazima kabla ya hapo watu watapata taarifa tu.   ā€œKwa sas...

Amber lulu amkana Ommy dimpoz mchana kweupe

Image
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu, ametaja list ya wasanii ambao amadai hawezi kutoka nao kimapenzi kwa namna yeyote ile.   Katika orodha hiyo Amber Lulu amemtaja msanii wa kwanza ambaye hawezi kutoka naye ni Dudubaya, Ommy Dimpoz, Alikiba na wengine wengi.   Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia kurasa za Facebook na YouTube za East Africa Television, Amber Lulu amesema, "siwezi kutembea na msanii kama Dudubaya anaongea sana, Kalapina yeye ni mkorofi sana, Ommy Dimpoz yeye hana habari na wanawake sijui kwanini".   Kwa sasa Amber Lulu anatamba na ngoma ya 'Haters' ambayo anatarajia kutoa video wiki ijayo

Msanii P didy atarajia mtoto na mrembo Lori harvey

Image
BAADA ya kuibuka tetesi kisha ikawa kweli, hatimaye mkongwe katika gemu la Hip Hop kutoka Marekani, P Diddy (49) anatarajia kupata mtoto kwa mrembo, Lori Harvey (22).  Ishu ya mkongwe huyo kutarajia kupata mtoto imekuja siku chache baada ya wawili hao kunaswa mapumzikoni huko Cabo, Mexico   Katika picha mbalimbali zilizosambaa mitandaoni, zinamuonesha Lori akiwa ameshika tumbo lake kama vile anaonesha ujauzito na nyingine zikimuonesha P Diddy akiwa amelishika tumbo la Lori.   Mwezi uliopita P Diddy aliungana na familia ya Lori pamoja na kukutana na wazazi wake wakati wapo mapumziko nchini Italia