Posts

Showing posts from September 8, 2019

Arsene wenger amshambulia vikali Mohammed Salah

Image
KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amemtaka straika wa Liverpool, Mohamed Salah kuacha uchoyo wakati akiichezea timu yake. Kauli ya Wenger imekuja siku chache baada ya Sadio Mane kukorofishana na Salah baada ya kunyimwa pasi wakati akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kwenye mechi dhidi ya Burnley.   Wenger, ambaye aliinoa Arsenal kuanzia 1996 hadi 2018, alidai kuwa Salah ameweka akili yake katika kuwaza ufungaji bora na kujikuta wakati mwingi ikiathiri kwenye maamuzi yake ya uwanjani.   Ulipotokea mzozo kwenye mechi ya Burnley ilibidi Jurgen Klopp atoe ufafanuzi huu ya suala hilo na kudai lilikuwa tukio dogo. Katika mchezo huo, ambao Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Mane alikasirishwa hatua ya Salah kutompa pasi wakati alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.   Mane alifoka vikali uwanjani kiasi cha kumlazimisha Klopp amtoe uwanjani staa huyo.   Wenger alisema kuwa Salah anatakiwa kujifunza kutoka kwa staa wa Barcelona, Lionel Messi. ā€œSalah ana...

Paul Makonda kumzawadiwa Juma kaseja milioni 10

Image
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeinga hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.   Mara baada ya Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa atampatia Mlinda Mlango wa Taifa Stars Tsh. Milioni 10.   Katika mchezo huo Mlinda Mlango Juma Kaseja Kadaka Penalti Moja, mbili kajipanga Burundi wakakosa.   "Kama tulivyoongea jana usiku wachezaji wote mmetimiza kiapo chenu cha jana nami nawaomba kwa muda wenu nitimize kiapo changu kwenu. Mwisho kila mchezo una nyota naomba nimpatie Milioni 10 Ndugu yetu Juma Kaseja kama nyota wangu wa leo," amesema RC Makonda.

Taifa stars yafuzu hatua ya makundi kwa kuichapa Burundi

Image
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuindosha Burundi kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Qatar 2022.   Mchezo wa leo umemalizika kwa goli 1-1, hata zilipoongezwa dakika 30 hakuna aliyeweza kuibuka mbabe ndipo mikwaju ya penalti ikaanza.   Tanzania ilipiga penalti tatu pekee zilizowapa ushindi huku Burundi wakikosa zote tatu walizopiga. Wafungaji wa Penalti kwa upande wa Tanzania ni Himid Mao, Erasto Nyoni na Gadiel Michael