Ukweli wema sepetu kuzimia na kupoteza fahamu usiku

Usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita Wema alianguka na kupoteza fahamu usiku wa manani akiwa kwenye sherehe yake ya kuzaliwa (private party) iliyofanyika nyumbani kwa dada yake, Nuru Sepetu maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar. Achana na tatizo la kukondeana linalozungumzwa na wengi, Risasi linafahamu kwamba hii ni mara ya tatu kwa mwanadashosti huyo kuzimia katika siku za hivi karibuni. Kufuatia tukio hilo la Jumapili kulizuka taharuki kubwa kwa wageni mbalimbali waliofika nyumbani hapo. Chanzo chetu makini kilisema kuwa, sherehe hiyo Wema alifanyiwa kwa kushtukizwa bila yeye kufahamu ambapo walioshiriki ni rafiki na ndugu wa karibu, jambo ambalo lilimfurahisha mno Wema na badaa ya kufurahi huku vinywaji vikiendelea ndipo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha. āUnajua Wema alikuwa na furaha iliyopitiliza na wakati wote hakupenda kukaa wala kufanya chochote, badala yake alikuwa akipita huku na huku kuzungumza na rafiki zake ndipo alipojisikia vibaya na kudondoka kis...