Posts

Showing posts from September 10, 2019

Yanga yatangaza kamati mpya ya hamasa mbotto na uwoya ndani

Image
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ameteua Kamati ya Kudumu ya Hamasa yenye wajumbe 21 ikiongozwa na Suma Mwaitenda katibu wake akiwa Deo Mutta.   Baadhi ya wajumbe walioteuliwa kuingia kwenye kamati hiyo ni Irene Uwoya, Jaquiline Wolper, Miriam Odemba, Flora Mvungi, Haji Mboto, Dominick Salamba, Hassan Bumbuli, Khamis Dacota, Jimmy Msindo na Jimmy Mafufu

Meneja wa Harmonize afunguka kuhusu ndoa ya Hamonize na Sarah

Image
Meneja wa msanii Harmonize, Beauty Mmari almaarufu kama Mjerumani, amepinga kuwa nyota huyo alifunga ndoa na mpenziwe Sarah Michelloti mnamo Ijumaa, Septemba 7 Picha za staa huyo wa wimbo maarufu wa 'Kadamshi' na mchumba wake aliyekuwa amevalia gauni lililoashiria wawili hao walikuwa wanafunga ndoa zilisambaa mitandaoni huku maelfu ya mashabiki zake wakimpongeza.    Kwa mujibu wa Nyakati.com, baadhi ya wafuasi wao mitandaoni walishangaa ni vipi nyota huyo alifanya harusi kisiri pasi na hata kuwaalika wasanii tajika kutoka Tanzania. Hata hivyo, meneja wa Harmonize, Mjerumani amepinga kwamba wawili hao walifunga ndoa na kusema kwamba Sarah alikuwa akiigiza katika wimbo ambao staa huyo anatarajia kuutoa hivi karibuni     "Harmonize hakufunga ndoa Jumamosi iliyopita, ila alimshirikisha mpenziwe kwenye video ya wimbo wake atakaoutoa hivi karibuni wa 'Marry Me'. Wazo nzima la wimbo huo ni sawia na lile Diamond alitumia na kumshirikisha Zari katika wimbo wake wa ...

Medie Kagere achaguliwa mchezaji bora wa mwezi August

Image
Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Agosti akiwashinda Lucas Kikoti wa Namungo na Seif Karihe wa Lipuli.   Naye Kocha wa Ruvu Shooting, Salum Mayanga amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo akiwashinda Mecky Mexime wa Kagera Sugar na Hitimana Thiery wa Namungo

Ratiba kamili ya michuano ya CAF champions league

Image
Ratiba kamili ya michuano ya mashindano ya klabu bingwa Afrika imetoka, klabu ya yanga ikiwa imepangiwa kukipiga na zesco united ya zambia ambapo yanga wataanzia ugenini mzunguko wa kwanza na kumalizia nyumbani mzunguko wa pili. Timu nyingine za hapa Tanzania zilizokua zikishiriki mashindano hayo simba,azam fc na kmc zilitolewa mapema kabisa kwenye hatua ya mtoano.

Jack Ma ajiondoa kwenye uongozi wa kampuni yake ya Alibaba

Image
Bilionea kutoka Hong Kong Jack Ma atangaza kustaa kuiongoza kampuni ya ALIBABA. Bilionea huyo aliyechochea biashara kupitia mtandao(Online) ameondoka rasmi katika nafasi ya Mwenyekiti Mkuu wa Kampuni ya Alibaba.   Hatua hii ya Jack Ma, inakuja ikiwa ni baada ya miongo miwili ya kuijenga kampuni hiyo hadi kufikisha kiasi cha Dola Bilioni 460 katika mzunguko wake wa biashara.   Katika sherehe yake ya kutimiza miaka 55, Jack Ma amesema anataka kujaribu kufanya mambo mapya katika sekta nyingine kabla hajafikisha miaka 70.   Kampuni ya Alibaba inajihusisha na kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao(Online) na ilianzishwa Aprili 4, 1999 kwa ushirikiano wa Jack Ma na Peng Lei.   ā€œKabla sijatimiza miaka 70, naweza kufanya kitu katika fani zingine, katika maeneo kama elimu,ā€ Ma alisema katika hafla ya Alibaba.   Ma alitangaza nia yake ya kujiuzulu mwaka mmoja uliopita. Hata baada ya kuachana na usimamizi na bodi ya wakubwa ya Alibaba, anatarajiwa kuendelea kuishauri kampun...

Lionel Messi ashinda tuzo ya mchezaji bora wa kimataifa

Image
Lionel Messi amepigiwa kura na kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Kimataifa kwa mwaka 2019, kwenye tuzo za ESPY.   Tuzo za ESPY (Excellence in Sports Performance Yearly Award) zinazolenga kutambua Utendaji bora wa wanamichezo kwa kila mwaka. Ni tuzo zinatolewa kwa sasa na kituo cha matangazo ya runinga Amerika (ABC) na hapo awali ESPN.   Ikubukwe Messi alikuwa mfungaji Bora: Laliga (Mabao 36), Uefa Champions League (Mabao 10) na mfungaji bora Ulaya (mabao 51).