Kim kardashian aingiza zaidi ya billioni 4 ndani ya dakika 8

Utajiri wa Familia isiyoishiwa na vituko ya The Kardashian sio tu Mamilioni ya watu ambao wanawafatilia kila mahala bali ni ushawishi walionao kwa hao watu, Inaripotiwa Kuwa Kim Kardashian Siku ya Jana (Sept. 10) ameingiza zaidi ya Tsh. Billion 4.5 ( $ 2M) Ndani ya dakika chache tu baada ya bidhaa zake mpya za nguo (SKIMS) kuanza kuuzwa. Bidhaa hizo mpya ndani ya siku moja tayari zimetajwa kuwa tishio kwa makampuni makubwa ya nguo za ndani za wanawake, Kampuni maarufu ya Spanx ilipata faida ya Dola Million 4 Mwaka wao wa Kwanza Lakini Kim K Tayari ameshaitengeneza nusu ya hizo Pesa ndani ya Dakika Tu. Hata Hivyo haishangazi sana ukiangalia na idadi ya watu wanaomfata kwenye Mitandao ya Kijamii, Kim K ana idadi ya Follower Million 147 Kwenye Instagram na Million 61.5 Kwenye Mtandao wa Twitter. TMZ wameripoti kuwa kabla ya #KimKardashian kuziachia rasmi hizo bidhaa za nguo za wanawake alilazimika kusogeza mbele hadi siku ya Jumanne (Septemba 10) kutokana na Mtandao ulio...