Posts

Showing posts from December 20, 2018

FAHAMU DALILI ZA TEZI DUME

Image
Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo.  Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo.  Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu.  Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi.  Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu wata...

MKE WA MUGABE KUKAMATWA NA POLISI AFRIKA KUSINI

Image
Waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa kwa mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe,Grace Mugabe, kutokana na tuhuma za kumshambulia mwanamitindo mwaka 2017, Polisi wameeleza.  Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuibatilisha kinga yake ya kidiplomasia mwezi Julai.  Serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bibi Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi.  Gabriella Engels alimshutumu kwa kumpiga katika chumba cha hoteli mjini Johannesburg.  Msemaji wa polisi,Vishnu Naidoo amesema ''Siwezi kuthibitisha kuwa hati ya kumkamata Grace Mugabe ilitolewa Alhamisi iliyopita''.  Alisema polisi wanatafuta usaidizi kutoka idara ya Interpol kufanyia kazi waranti hiyo. Haijafahamika kwa nini ripoti kuhusu waranti hiyo ilicheleweshwa na hakuna tamko lolote lililotolewa na Bibi Mugabe au mamlaka za Zimbabwe.  Familia ya Mugabe inamiliki mali nchini Afrika Kusini  Tukio la mashambulizi dhidi ya mwanamitindo lilitokea miezi mi...