Posts

Showing posts from January 7, 2019

ZITTO KABWE ANA HOFU JUU YA USALAMA WAKE

Image
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anahofia usalama wake kutokana na taarifa alizozipata, akisema kuna mpango wa kumdhuru.  Kiongozi huyo wa upinzani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia agenda za muungano wa vyama 10 vya upinzani kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, alieleza kupitia mtandao wa Twitter, akionya wale walionuia kumdhuru.  Katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe ameandika: ā€œTunafahamu kuwa Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ā€˜ Vita ya Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI( mie huyo). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha. SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslaniā€ alisema katika ukurasa huo.

MAGAZETI YA LEO 08/01/2019

Image