Mbwana Samatta mtanzania wa kwanza kucheza na kufunga goli UEFA

Ni historia mbili mpya Mbwana Samatta ameandika usiku uliopita. Amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano ya Klabu bingwa Ulaya na pia wa kwanza kufunga goli kwenye michuano hiyo. Hata hivyo, furaha yake ya kuweka rekodi binafsi imegubikwa na matokeo mabaya baada ya klabu yake ya KRC Genk kupokea kipigo kizito cha goli 6-2 kutoka kwa RB Salzburg. Samatta alipachika bao lake wavuni katika dakika ya 52, lakini halikuweza kubadili mwelekeo wa mchezo sababu mpaka muda huo walikuwa nyuma kwa goli 5-1. Awali kulikuwa na hofu juu ya afya ya Samatta na iwapo angecheza mechi hiyo baada ya kuumia goti alipokuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi Hivi Karibuni. Hata hivyo majeraha hayo madogo yalipona kabla ya mchezo wa jana usiku ambapo alicheza kwa dakika 85. Mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Genk alikuwa mshambuliaji Erling Braut Håland aliyepachika magoli matatu katika dakika ya dakika ya 2',34' na 45'. Katika mchez...