Billnas apinga kupewa gari na Nandy

MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, William Lyimo āBillnassā ameibuka na kufungukia madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amepewa gari na aliyekuwa mpenzi wake, Faustina Charles Mfinanga āNandyā kwa kusema hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo. Akipinga na Risasi Jumamosi, Billnass alisema ameyaona maneno hayo mitandaoni watu wakidai kuwa Nandy amemnyangāanya gari aina ya Toyota Crown mpiga picha wake na kumpatia yeye kitu ambacho hakina ukweli, yeye anayo magari yake mawili. āUnajua watu wanapenda sana kuongea ukiangalia gari langu na la yule mpiga picha ni tofauti kabisa, watu wanaongea vitu wasivyovijua,ā alisema Billnass. Aidha, Billnass alisema kuwa yeye anamiliki magari mawili ambayo yote ana kadi zake zinazosoma jina lake. āMimi ninamiliki magari mawili siwezi kupewa gari na Nandy tena ambalo ameshampa mtu zawadi,ā alisema Billnass. Billnass na Nandy kwa sasa wamekuwa habari ya mjini kufuatia kuachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Bugana ambao ...