Posts

Showing posts from September 16, 2019

Kikosi cha Taifa stars kinachoshiriki michuano ya CHAN

Image
Hiki hapa kikosi cha wachezaji 25 waliochaguliwa kushiriki michuano ya CHAN kwenye mchezo dhidi ya Sudan

Hamza Bin laden mtoto wa Osama auawa na jeshi la marekani

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliuawa katika operesheni ya Marekani.   Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.   Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita. Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.   Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.   ''Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan / Pakistan''.Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu ya Whitehouse.  

Azam Fc yachezea kichapo kombe la mabingwa Afrika

Image
Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United wamepoteza kwa kukubali kufungwa goli 1 kwa bila.   Bao pekee la Triangel United ya Zimbabwe lilifungwa dakika ya 34 na Ralph Kawondera kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa Azam FC.   Licha ya Azam FC kupewa sapoti kubwa na mashabiki waliojitokeza uwanja wa Azam Complex hayakuzaa matunda kwani safu ya ulinzi ya Triangle United ilikuwa ngumu na ikajilinda na hatari zote.   Sasa Azam FC ina kazi nzito ya kwenda kutafuta matokeo ugenini kwenye mchezo wa marudiano unaoatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27-29 nchini Zimbabwe.

Rayvanny kumzima Harmonize baada ya kuondoka WCB

Image
TANGU kuondoka kwa mwanamuziki Rajab Abdul ā€˜Harmonize’ kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) kuna harakati za ndani zinazofanywa kumpaisha memba mwingine wa kundi hilo, Raymond Mwakyusa ā€˜R ayvanny’.   Habari za chini ya kapeti zilieleza kuwa, mwaka huu wa 2019 huenda ukamalizika kwa mafanikio makubwa kwa Rayvanny kutokana na ā€˜fujo’ zinazofanyika za kumpaisha kimataifa.   Ilielezwa kuwa, kasi yake ya kufanya kolabo za kimataifa ni kubwa kama aliyokuwa nayo Harmonize au Harmo alipokuwa ndani ya lebo hiyo.   Mpaka sasa Rayvanny ameshafanya kolabo na wanamuziki wakubwa duniani kama Pitbull, Jason Derulo na Nora Fatehi.   Habari nyingine nzito ni kwamba kwa sasa Rayvanny yupo kwenye maandalizi ya kolabo na mwanamuziki aliyewahi kufanya kazi chini ya lebo ya rapa mkubwa duniani, Jay-Z kupitia lebo yake ya Roc Nation anayefahamika kwa jina la Philly Freeway.   Kwa mujibu wa prodyuza maarufu wa Bongo Fleva, S2kizzy, Rayvanny na jamaa huyo tayari wameingia studio...