Posts

Showing posts from December 18, 2018

CHARZ BABA AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE MARIAM

Image
Msanii kutoka katika bendi ya Twanga pepeta Charles Baba amefanya sherehe Jumamosi hii na mpenzi wake ambaye alifahamika kwa jina la Mariam na ni baada ya kudumu naye kwa takribani miaka kumi katika uchumba wao.  Amezungumza hayo ndani ya eNewz huku akisisitiza kwamba hayuko tayari kuongea suala lolote kuhusu ndoa zake zilizopita kwa sasa kipaumbele chake ni mke wake Mariam na kusema kwamba anampenda sana na hawezi kumuacha kamwe.  "Nampenda sana mume wangu ni chaguo langu na nimempenda mwenyewe siwezi kubadilisha mawazo yangu na napenda watu wafahamu kwamba nimekuwa katika mapenzi na mme wangu tangu mwaka 2005 mpaka sasa hivyo namfahamu vizuri na mimi ni shabiki wa kazi zake" aliongea mke wa Charles Baba.  Charles Baba amemalizia kwa kusema kwamba pamoja na kwamba imezoeleka kwa wasanii wakioa wanapotea katika muziki lakini kwa upande wake hawezi kuacha muziki kwa kuwa ndio kazi yake lakini pia mke wake amekuwa akimsapoti kwa kiasi kikubwa katika kazi yake hiyo

KOCHA JOSE MOURINHO AFUKUZWA KAZI MANCHESTER UNITED

Image
Kocha Jose Mourinho amefutwa kazi na Manchester United ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.  Man United kupitia taarifa yake imeeleza kuwa imefikia uamuzi huo ili kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.  "Klabu inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye'', imeeleza taarifa ya klabu.  Kiungo wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa msimu huu wa 2018/19. 

WAFANYABIASHARA MITANDAONI WATAKIWA KULIPA KODI

Image
Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote. Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere jana asubuhi alipokuwa akizungumza kupitia Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza mapato. Kamishna Kichere alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji kuhusu uwepo wa watanzania wachache wanaolipa kodi (zaidi ya milioni 2) wakati jumla ya Watanzania wapo takribani milioni 55. Akizungumzia mkakati wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi, kamishna huyo alisema wameanza kuwafikia watu wanaofanya biashara mitandaoni ambao wamekidhi vigezo vya kutakiwa kulipa kodi, wawe wanalipa kodi kama wafanyabiashara wengine. Alieleza kuwa, wafanyabishara ambao thamani ya biashara zao ni zaidi ya shilingi milion...

DIAMOND NA TANASHA KUWEKA SIRI MAHUSIANO YAO

Image
Mpenzi mpya wa Diamond Platinumz, Tanasha amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa wameamua kuweka siri mahusiano yake ya kimapenzi na Diamond Platinumz na si kama apo awali walivyokua wanajiachia kwenye mitandao ya kijamii.  Kauli ya Tanasha imekuja siku chache baada ya Diamond kutangaza tarehe ya kufunga ndoa na mrembo huyo kutoka Kenya.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanadada huyo ameandika haya:  Just to make things clear... D and I came to a mutual understanding that it may be too soon to be public with our relationship on social media right now. So we decided to keep our relationship private for the moment until we feel like going public again. May God bless you all .šŸ™ā¤ļø