BABA AKAMATWA NA POLISI KWA KUMUUA MWANAE

Hazra Mwasenga, mkazi wa Kitongoji cha Haduye Kijiji cha Iwala, Kata ya Itale wilayani Ileje, mkoani Songwe, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mwanawe, Subi Mwasenga (28), kwa kumkata mapanga kisha kumzika kienyeji kwa siri, akimtuhumu kuiba nyama. Mwenyekiti wa kijiji hicho, Joseph Mwabezya, alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki na aligundua alipotembelea maeneo ya makazi ya mzee huyo alimsalimia na kuuliza kuwa mwanawe haonekani na kuhoji tuta lililopo pembezoni mwa nyumba yake. Alisema baada ya kuhoji, Mwasenga alimweleza kuwa lile tuta ni kaburi la mwanawe ambaye alimuua kwa kumkata na panga kwa kosa la kuiba nyama na kwenda kuiuza, wakati yeye alichinja ngāombe mdogo kwa ajili ya kitoweo. Alisema baada ya kumkata na mapanga mwanawe, alipoona amekufa aliamua kuchimba shimo na kumfukia kwa siri kwa kuwa alitenda kosa la kuiba nyama. āāNakuomba mwenyekiti nimekueleza haya kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, iwe siri usimwambie mtu,ā alisema mwenyekiti...