Posts

Showing posts from December 14, 2018

NJIA ZA KUTUNZA NYWELE ZAKO KIURAHISI ZAIDI

Image
. Kwanza kabisa unatakiwa kuosha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair (nywele asili) au kama utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa basi jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha.  2. Pili ni kupaka mafuta nywele zako, zifanye nywele zako zivutie kwa kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa.  3. Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45...

MAGAZETI YA LEO 15/12/2018

Image

KANGI LUGOLA AGEUKIA MAKANISA NA MISIKITI

Image
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kuna baadhi ya watu ambao wanajipenyeza kupitia mgongo wa taasisi za dini kujifanya wahubiri kumbe ni wachochezi na wanajiingiza katika masuala ya kisiasa.  Amesema wizara yake iko makini katika kusajili makanisa na misikiti yote nchini na kwamba mpaka sasa imepokea maombi mengi ambayo yametumwa kuomba usajili.  Lugola aliyasema hayo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Sunsi, Kata ya Nampindi, Mwibara, Bunda mkoani Mara.  Alisema baadhi yao waombaji hawajapata usajili kwa sababu wanahitaji umakini mkubwa katika kufanya uchunguzi wa kina kabla hawajatoa usajili na kwamba lengo ni kuepusha baadhi ya taasisi za dini zenye mpango mbaya na maendeleo ya  nchi.   Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara, alisema taasisi za dini zina mchango mkubwa nchini na uwapo wao ni muhimu katika maendeleo ya nchi na serikali inauthamini mchango wao katika kuimarisha amani na kuwaweka watu pamoja....

YOWERI MUSEVENI AKATAA KUACHIA MADARAKA NCHINI UGANDA

Image
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amewaambia wazi wapinzani wake kuwa hana mpango wa kuachia madaraka hivi karibuni, hivyo waachane na mawazo yao ya kuwaza kiti hicho.   Rais Museveni ameyasema hayo kwenye mkutano wa ndani wa chama ambao uliwakusanya pamoja viongozi wa vyama vilivyopo Bungeni, mkutano uliofanyika Jijini Kampala.  Museveni amesema amefurahia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo, ambapo aliwaambia wapinzani wake kwamba hatofikiria kubadilishana madaraka mpaka pale atakaporidhishwa na Ustawi na usalama wa kimkakati wa nchi za Afrika.  ā€œNasikia watu kama Mao wanazungumzia kuachia madaraka, ni kwa namna gani watakaa kwenye umati na kumuona Museveni akikabidhi madaraka. Hicho ndicho kitu muhimu kwake. Sidhani kama ni sahihi kwa yeye kusema hivyo, badala ya kuzungumzia hatma ya Afrika, mnaongelea vitu visivyo na maana, uchaguzi, nani atakuwa nani. Na ndio kwa sababu nilisema kama bado nina nguvu nitaendeleaā€, amesema Rais Museveni k...

TFF YAKATA RUFAA KUPINGA WAMBURA KURUDI KWENYE UONGOZI

Image
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limekata Rufaa Mahakamani kupinga hukumu ya kumrejesha madarakani makamu wa Rais Michael Wambura ambaye amefungiwa maisha.  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Desemba 14, 2018, kwenye makao makuu ya TFF, katibu mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidau amesema kesi hiyo itasimamiwa na wakili msomi Alex Mgongolwa.  Michael Wambura alichaguliwa kuwa makamu wa Rais kwenye uchaguzi wa TFF Agosti 12, 2017 jijini Dodoma.  Machi 15, 2018, Wambura alifungiwa maisha kutojihusisha na soka. Machi 25, Kamati ya Utendaji ya TFF, ilimteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi  ya makamu wa rais wa TFF.  Novemba 30 alirudishwa kazini na mahakama ya rufaa baada ya kubaini kuwa hana makosa. Desemba 4 Wambura alikwenda TFF kupeleka barua ya mahakama lakini hakukuta kiongozi yoyote.  Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye leo shirikisho limeamua kuweka wazi kuwa hawawezi kufanya kazi na Wambura hivyo wamekata rufaa kupinga maamuzi ya mahakam...

WEMA SEPETU KUFUNGUA DUKA LA MAHITAJI YA WATOTO

Image
Baada ya kimya cha muda mrefu mtandaoni, muigizaji wa Filamu nchini, Wema Sepetu amerudi kwa kishindo katika ukurasa wake wa Instagram.  Wema baada ya akaunti yake kudaiwa kudukuliwa, msanii huyo amerejea na kufungua kwa duka lake la Little 'Sweet Hearts'  Pia msanii huyo ameweka wazi ujio wa filamu inayokwenda kwa jina la ' Saa Mbovu' ambayo ameshirikiana na Prince HDV pamoja na Aunt Ezekiel. 

KIVUKO KIMEZAMA NA KUUA WATU TISA

Image
Mashua iliyokuwa imebeba abiria imezama na kusababisha vifo vya watu tisa kusini mwa nchi ya Nigeria..  Kulingana na vyombo vya haabri nchini humo,mashua hiyo ilikuwa imebeba abiria 140  katika mto wa Benue.  Mashua hiyo imeripotiwa kuzama kutokana na kutokea kwa dhoruba kali.  Kati ya waliopoteza maisha wanne kati yao ni watoto  Inasemekana mashua ilibeba abiria  na mizigo kuzidi uwezo wake.

MBWANA SAMATTA AMTAJA ROLE MODEL WAKE

Image
Nahodha wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta amefunguka juu ya historia ya maisha yake ya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi katika klabu hiyo.  Alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa klabu ya Genk, Samatta amesema kuwa alianza kucheza soka tangu alipokuwa mtaani Jijini Dar es salaam ambapo katika kipindi hicho alishindwa hata kumudu kununua jozi ya kiatu cha kuchezea.  Ameendelea kusema kuwa kwenye nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania hakuna 'Academy' za kuweza kuwaandaa vijana kucheza soka kwa ubora na kutimiza ndoto zao za maisha kama ilivyo kwa mabara mengine, isipokuwa kwa juhudi binafsi ambazo wachezaji wachache ndio wanaoweza kufanya hivyo.  Kuhusu mazingira ya soka nchini Tanzania na mchezaji gani ambaye yeye anamuiga na anayetamani kufanana naye (Role model), Samatta amesema, "mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania wanapenda sana kutazama EPL na mimi nilikuwa mmoja wao, pindi nilipokuwa nikimtazama Thierry Henry nlikuwa najisemea mwenye...

OBREY CHIRWA ATUA MAKAO MAKUU YA YANGA

Image
Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa, jana Alhamisi aliibukia Makao Makuu ya Klabu ya Yanga kwa ajili ya kushughulikia baadhi ya mambo yake na klabu hiyo.  Chirwa aliwahi kuitumikia Yanga kwa misimu miwili alipojiunga nayo msimu wa 2016/17 akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa timu hiyo.  Mshambuliaji huyo alitua klabuni hapo majira ya mchana ambapo alikutana na viongozi kadhaa wa Yanga na kujadili juu ya mambo yake, kabla ya kuondoka kwa kutumia usafiri wa gari aina ya Toyota IST.  Pamoja na kukutana na viongozi wa timu, pia straika huyo alikutana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambapo waliongea kwa muda ingawa haikufahamika walizungumza nini.  Chirwa ambaye msimu uliopita alifunga mabao 12 akiwa na Yanga, aliondoka ndani ya kikosi hicho na kutimkia Nogoom FC ya Misri, kisha akarejea Tanzania na kutua Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.