Posts

Showing posts from September 6, 2019

Mtangazi Mboni Masimba afunga ndoa leo jijini dar es salaam

Image
Mrembo na mtangazaji wa muda mrefu nchini, Mboni Masimba amefunga ndoa leo na mpenzi wake Ally Tajiri, ambaye sasa amekuwa mume wake.   Ndoa hiyo imefungwa kwa siri leo Septemba 6, 2019, Masaki jijini Dar es salaam na kuhudhuria na marafiki wa karibu wa Mboni.   Mpenzi wake huyo anayefahamika kwa jina la Ally Tajiri, imeelezwa kuwa muda mwingi anaishi nchini Uingereza, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Mboni kuhamia nchini humo kwaajili ya kuanza maisha ya ndoa na familia.  

Yanga wagoma kuweka nembo nyekundu kwenye jezi zao kutoka kwa mdhamini wa ligi

Image
Timu ya yanga wamegoma kuweka nembo nyekundu kwenye jezi zao, nembo ambayo ni ya mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara Vodacom. Yanga imesema kua hawawezi kufanya hivyo kwasababu wana katibu ya timu na hairuhusu kuweka nembo au rangi nyekundu kwenye jezi zao.  Tazama video 

Wachezaji bora wa FIFA miaka iliyopita

Image
Orodha ya wachezaji bora wa FIFA kwa miaka 10 iliyopita,Ronaldo na Messi waongoza kuchaguliwa miaka mingi kuanzia mwaka 2009 hadi 2018.

Wachezaji wanaowania kikosi bora cha Fifa 2019

Image
List ya wachezaji wanaowania kikosi bora cha Fifa mwaka 2019 (Fifa world pro 2019). 1.Viungo wanaowania 2.Washambuliaji wanaowania 3.Walinda mlango wanaowania 4.Mabeki wanaowania

Robert Mugabe afariki dunia

Image
Rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Familia ya rais huyo wa zamani imeiambia BBC kuwa amefariki akipigania afya yake, ambapo alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa amemzungumzia mzee Mugabe katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ni kiongozi shupavu na aliyeongoza vita ya kupinga ukoloni pamoja na kuwapigania watu wake. Cde Mugabe was an icon of liberation, a pan-Africanist who dedicated his life to the emancipation and empowerment of his people. His contribution to the history of our nation and continent will never be forgotten. May his soul rest in eternal peace (2/2) Robert Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 katika nchi iliyojulikana kama Rhodesia ambayo sasa ni taifa la Zimbabwe. Katika historia yake ya mapambano ya kuipigania nchi hiyo, Mugabe aliwahi kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 10 baada ya kuikosoa serikali ya kikoloni ya Rhodesia mwaka 1964. Baada ya kuiong...