MSANII NIKKI WA PILI NA MCHUMBA WAKE WAPATA MTOTO

Msanii wa muziki Bongo, Nikki wa Pili na mchumba wake wamejaliwa kupata mtoto wa kike siku ya jana. Rapa huyo kutoka kundi la Weusi ameeleza kuwa wamempataia mtoto wao huyo jina la Zuri. kupitia mtandao wa Twitter ameandika; "Namshukuru Mwenyezi Mungu jana katujalia binti tumempa jina anaitwa Zuri, pili namshukuru mama zuri, safari ya kuja kwake imenifunza mengi sana, ule mchakato wa kujifungua umefanya nizidishe mara 10000 upendo wangu na heshima yangu kwa wanawake wote duniani," ameeleza Nikki. Utakumbuka December mwaka jana Nikki wa Pili alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo ikiwa ni wiki kadhaa tangu Bibie kuhitimu elimu yake ya Chuo Kikuu.