Posts

Showing posts from 2018

FAHAMU DALILI ZA TEZI DUME

Image
Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo.  Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo.  Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu.  Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi.  Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu wata...

MKE WA MUGABE KUKAMATWA NA POLISI AFRIKA KUSINI

Image
Waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa kwa mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe,Grace Mugabe, kutokana na tuhuma za kumshambulia mwanamitindo mwaka 2017, Polisi wameeleza.  Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuibatilisha kinga yake ya kidiplomasia mwezi Julai.  Serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bibi Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi.  Gabriella Engels alimshutumu kwa kumpiga katika chumba cha hoteli mjini Johannesburg.  Msemaji wa polisi,Vishnu Naidoo amesema ''Siwezi kuthibitisha kuwa hati ya kumkamata Grace Mugabe ilitolewa Alhamisi iliyopita''.  Alisema polisi wanatafuta usaidizi kutoka idara ya Interpol kufanyia kazi waranti hiyo. Haijafahamika kwa nini ripoti kuhusu waranti hiyo ilicheleweshwa na hakuna tamko lolote lililotolewa na Bibi Mugabe au mamlaka za Zimbabwe.  Familia ya Mugabe inamiliki mali nchini Afrika Kusini  Tukio la mashambulizi dhidi ya mwanamitindo lilitokea miezi mi...

CHARZ BABA AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE MARIAM

Image
Msanii kutoka katika bendi ya Twanga pepeta Charles Baba amefanya sherehe Jumamosi hii na mpenzi wake ambaye alifahamika kwa jina la Mariam na ni baada ya kudumu naye kwa takribani miaka kumi katika uchumba wao.  Amezungumza hayo ndani ya eNewz huku akisisitiza kwamba hayuko tayari kuongea suala lolote kuhusu ndoa zake zilizopita kwa sasa kipaumbele chake ni mke wake Mariam na kusema kwamba anampenda sana na hawezi kumuacha kamwe.  "Nampenda sana mume wangu ni chaguo langu na nimempenda mwenyewe siwezi kubadilisha mawazo yangu na napenda watu wafahamu kwamba nimekuwa katika mapenzi na mme wangu tangu mwaka 2005 mpaka sasa hivyo namfahamu vizuri na mimi ni shabiki wa kazi zake" aliongea mke wa Charles Baba.  Charles Baba amemalizia kwa kusema kwamba pamoja na kwamba imezoeleka kwa wasanii wakioa wanapotea katika muziki lakini kwa upande wake hawezi kuacha muziki kwa kuwa ndio kazi yake lakini pia mke wake amekuwa akimsapoti kwa kiasi kikubwa katika kazi yake hiyo

KOCHA JOSE MOURINHO AFUKUZWA KAZI MANCHESTER UNITED

Image
Kocha Jose Mourinho amefutwa kazi na Manchester United ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.  Man United kupitia taarifa yake imeeleza kuwa imefikia uamuzi huo ili kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.  "Klabu inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye'', imeeleza taarifa ya klabu.  Kiungo wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa msimu huu wa 2018/19. 

WAFANYABIASHARA MITANDAONI WATAKIWA KULIPA KODI

Image
Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote. Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere jana asubuhi alipokuwa akizungumza kupitia Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza mapato. Kamishna Kichere alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji kuhusu uwepo wa watanzania wachache wanaolipa kodi (zaidi ya milioni 2) wakati jumla ya Watanzania wapo takribani milioni 55. Akizungumzia mkakati wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi, kamishna huyo alisema wameanza kuwafikia watu wanaofanya biashara mitandaoni ambao wamekidhi vigezo vya kutakiwa kulipa kodi, wawe wanalipa kodi kama wafanyabiashara wengine. Alieleza kuwa, wafanyabishara ambao thamani ya biashara zao ni zaidi ya shilingi milion...

DIAMOND NA TANASHA KUWEKA SIRI MAHUSIANO YAO

Image
Mpenzi mpya wa Diamond Platinumz, Tanasha amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa wameamua kuweka siri mahusiano yake ya kimapenzi na Diamond Platinumz na si kama apo awali walivyokua wanajiachia kwenye mitandao ya kijamii.  Kauli ya Tanasha imekuja siku chache baada ya Diamond kutangaza tarehe ya kufunga ndoa na mrembo huyo kutoka Kenya.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanadada huyo ameandika haya:  Just to make things clear... D and I came to a mutual understanding that it may be too soon to be public with our relationship on social media right now. So we decided to keep our relationship private for the moment until we feel like going public again. May God bless you all .šŸ™ā¤ļø  

MAGAZETI YA LEO 17/12/2018

Image

WAZIRI MKUU CASSIM MAJALIWA AFUNGUA CHANELI YA UTALII

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli mpya ya utalii inatarajiwa kuvutia watalii wengi zaidi kuja nchini sambamba na kuongeza pato la taifa.  Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipokuwa akizindua chaneli hiyo ya utalii inayojulikana kama ā€œTanzania Safari channelā€ Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli hiyo mpya itatoa fursa ya kutangaza wanyama mbalimbali waliopo katika hifadhi za wanyama, utamaduni wa watanzania pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kuvutia watu wengi zaidi kuja kufanya utalii na hatimaye kuongeza kiasi cha fedha kitachochangia katika pato la taifa.  ā€œChaneli hii ni njia muhimu ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi yetu, ambapo itaongeza idadi ya watu watakaotembelea Tanzaniaā€ alisema Waziri Mkuu Majaliwa  Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa kwa sasa watalii wanaokuja nchini kwa mwaka ni milioni 1.3 , na matarajio ya Serikali ni kuon...

SABABU ZA UKE KUTOA HARUFU HIZI HAPA

Image
Ni matumaini nyote mnaendelea vyema, nami alhamdulillah ala kul Hali naendelea vyema  Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu na ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni, leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK,  -Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo  -Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huviking...

SAUTI SOL WATHIBITISHA KUFANYA COLLABO NA HARMONIZE

Image
Kundi la Muziki la Sauti Sol kutoka nchini Kenya wamethibitisha kufanya kolabo la Harmonize.  Sauti Sol wamesema kuwa tayari msanii huyo alivyokuja Nairobi wakampigia wakaingia studio kwasasa kilichobaki ni kufanya video.  "Harmonize ni rafiki yetu alikuwa amekuja Nairobi akatupigia tulikua tukiambia kuwa tutafanya nyimbo all the time lakini hatukupata nafasi, this time alitupigia tulikuwa area tukampigia tuaingia studio akaua verse sasa hivi tunataka kushoot video kati ya huu mwaka au next year," Wamesema Sauti Sol walipowasili nchini

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA NKANA FC LEO

Image
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Nkana Red Devils, Caf Champions League.  1. Aishi Manula  2. Nicolas Gyan  3. Mohamed Hussein  4. Pascal Wawa  5. Erasto Nyoni  6. James Kotei  7. Jonas Mkude  8. Clatous Chama  9. John Bocco  10. Meddie Kagere  11. Emmanuel Okwi