Posts

Showing posts from May, 2019

MBOWE AFUNGUKA LOWASSA KUONDOKA UKAWA

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amezungumza kwa mara ya kwanza kwa undani kuhusu kile anachodai ni sababu ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015, Edward Lowassa kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni Singida Kaskazini, Mbowe alisema kuwa Lowassa alihama baada ya kushindwa kuhimili mikiki-mikiki ya upinzani.  Mbowe alisema kuwa Lowassa alishindwa kutoa matamko kadhaa kama mgombea urais wa chama hicho hata baada ya kukatazwa kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wapiga kura milioni sita waliomuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu.  Alikumbushia kuwa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu alikaa kimya baada ya kupata misukosuko iliyotokana na kauli aliyoitoa mwaka 2017 akitaka masheikh wanaoshikiliwa gerezani kuachiwa huru au kushtakiwa kama wana makosa, kauli iliyomsababisha kuhojiwa polisi.  Mbowe anadai kuwa Lowassa alimpigia simu akionesha k...

WAZIRI KANGI LUGOLA ATOA ONYO KWA ASKARI POLISI

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema hatamvumilia askari au mtumishi aliyeopo chini ya wizara hiyo iwapo atabainika anamnyanyasa, kumtishia au kumsumbua mwekezaji anayefuata sheria  ikiwamo kulipa kodi.  Lugola amesema hayo mjini Morogoro alipozungumza na viongozi wa Kampuni ya Tumbaku ya Tanzania Leaf.  Amesema askari atakayebainika kufanya hivyo sheria dhidi yake itachukua mkondo wake kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wawekezaji kuonewa na baadhi ya vyombo vya ulinzi bila sababu, huku wakitishiwa na kuapa kuwa atakayebainika atamfukuza kazi mara moja.  Pia, amesema hivi karibuni uongozi wa kampuni hiyo uliwasilisha malalamiko kwa ofisi ya Waziri Mkuu kutokana na viongozi wake wakuu kunyanyaswa na kutishiwa kukamatwa na polisi mkoani Morogoro.  Lugola amesema Serikali imedhamiria kufikia uchumi wa kati kwa sekta ya viwanda na kwamba, imetoa nafasi kubwa kwa wawekezaji kuwekeza nchini kwa kufuata sheria zilizopo.  ā€œLakini kumeku...

RAIS MAGUFULI AWAPA ONYO WAFANYABIASHARA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za vyakula katika msimu huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.  Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo wakati akihutubia maelfu ya Watanzania waliofika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kushuhudia mashindano maalumu ya 20 ya kusoma Qur'aan tukufu barani Afrika, yanayoandaliwa na taasisi ya AL-hikma ya nchini Tanzania.  Magufuli amesema kuwa kitendo cha kupandisha bidhaa hizo hakimpendezi mwenyezi Mungu kwani mfanyabiashara hawezi kutajirika kwa kipindi cha mwezi mmoja, bali ni kujichumia dhambi.  ā€œNatoa wito wa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei za bidhaa ambazo zinatumiwa na ndugu zetu Waislamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, mamlaka za serikali zifuatilie suala hili kwa karibuā€, amesema Rais Magufuli.  Ameongeza kuwa, "kufunga katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan au Kwaresma bila ya kuyaishi maneno yaliyo kwenye vitabu vitakatifu ni kazi bure, so...