HUMPHREY POLEPOLE AONGEA KUHUSU BERNAD MEMBE
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Humphrey Polepole amesemaa si kweli kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ally alimuitwa Bernard Membe kupitia mitandao.
Polepole ameyasema hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kupitia Clouds TV ambapo amesema kwanza ifahamike CCM ilishafunga huo mjadala na haitaki kuuongelea tena.
"Katibu Mkuu alikuwa kwenye kikao cha ndani (Hakumuita Membe mitandaoni kama inavyosemwa)," amesema Polepole.
Aliongeza kuwa 'Taarifa iliyotolewa nje ilitolewa kimakosa', amesema Polepole na kueleza kwamba CCM iliona ni busara kuachana na suala hilokwa sababu lilipotoshwa kwa kiwango kikubwa.
Comments
Post a Comment