Kiongozi wa islamic state auawa na vikosi vya marekani



Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuuawa kwa kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) kaskazini magharibi mwa Syria, Trump amesema Abu Bakr al-Baghdad alijilipua wakati alipozingirwa na kikosi maalum cha Marekani. 

Amesema kuwa amekufa kama Mtu muoga na kama Mbwa. Abu Bakr al Baghdad hakuonekana hadharani tangu mwaka 2014. 

Amejiua kwa mabomu aliyokuwa ameyavaa mwilini mwake. Washirika wake kadhaa pia wameuawa katika shambulio hilo lililofanywa na vikosi vya Marekani 

Amemtangaza Baghdad kama msumbufu na kiongozi wa Kundi la Kigadi aliyekuwa akisakwa zaidi kwa sasa Ulimwenguni.

Comments