Posts

Showing posts from January, 2019

HARMONIZE KUKAMATWA NA POLISI KISA BANGI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema ameongea na Gavana wa Ghana kumchunguza msanii, Harmonize ambaye yupo nchini humo kama anatumia bangi ili kama ni kweli akirudi amuweke rumande.  Hatua hiyo imekuja baada ya Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.  "Nimemuona mtu mmoja yuko Ghana kule ule moshi unavyotoka ni kama wa Bangi na tayari nimeshaongea na rafiki angu Gavana wa Ghana pale wanisaidie kumfuatilia Harmonize anatumia Bangi au sigara na kama anatumia bangi akitua hapa ni Lock Up moja kwa moja namna unavyojithaminisha ndivyo serikali itakavyo kuthamini," alisema Makonda.  Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019  wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. 

BILLNAS KUJA NA COLLABO NA ALIKIBA

Image
Msanii wa Muziki, Bill Nas amefunguka kuhusu ujio wa kolabo yake na AliKiba.  Bill Nass akiongea katika kipindi cha The PlayList cha Times FM amesema kuwa kolabo na msanii huyo tayari wameshafanya.  "Kolabo na Alikiba ipo na tayari tumeshafanya bado kutoka kwasababu ya taratibu zao kwasababu Ali yuko chini ya Sony hata kutoa ngoma pia kuna utaratibu wake, nasubiri tu utaratibu wao kama itatoka mwakani au mwaka huu," alisema Bil Nass.  Billnass kwasasa anatamba na kibao cha wimbo wake mpya unaoitwa 'Funga Geti' aliomshirikisha Roma ambao mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube una 366,181 views. 

THIERRY HENRY MBIONI KUTIMULIWA MONACO

Image
Klabu ya soka ya Monaco ipo mbioni kumtimua kazi legendari wa timu ya Arsenal, Thierry Henry kutokana na matokeo mabovu anayoendelea kuyapata.  Henry huwenda akatimuliwa baada ya kuiyongoza klabu hiyo inayoshiriki Ligue 1, tangu mwezi Oktoba.  Mwishoni mwa wiki iliyopita Monaco ilikubali kipigo cha mabao 5 – 1 dhidi ya Strasbourg na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi.  Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa Monaco huwenda wakamrudisha aliyekuwa kocha wake, Leonardo Jardim ambaye nafasi yake ilirithiwa na Thierry Henry.  Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 1998 amejikuta akiingia kwenye majanga tangu kuanza kazi yake ya ukocha kwa mara ya kwanza baada ya kushinda mechi miwili pekee kwenye michezo 12 aliyoiongoza Monaco huku akishindwa kupata hata ushindi mmoja kwenye uwanja wa nyumbani wa Stade Louis II.

RAIS MNANGAGWA AREJEA NCHINI ZIMBABWE KUTOKA KWENYE ZIARA

Image
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.  Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.  Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.  Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic ChangeNelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.  Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitisha, Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo amekamatwa pia, Amesema vyombo vya ulinzi vimekuwa vikikamata familia za watu majumbani mwao. 

CRISTIANO RONALDO AKUBALI KULIPA FAINI YA BILIONI 50 BAADA YA KUKWEPA KULIPA KODI

Image
Mchezaji wa Timu ya Juventus Cristiano Ronaldo amekubaliana na mamlaka za Hispania kulipa faini kuhusu  kesi yake ya ukwepaji kodi.  Msemaji wa mahakama amethibitisha kwamba Ronaldo atalipa faini na kuepuka kifungo cha miaka miwili  jela.  .  Hii inatokana na kwamba sheria za Hispania zinatoa nafasi kwa mtuhumiwa  kuchagua adhabu ya  jela au kulipa faini akipatikana na hatia  ya kosa la kwanza.  Ronaldo atalipa takribani pauni milioni 17 zaidi ya shilingi bilion 49 za kitanzania alituhumiwa kukwepa kulipa kodi ya mapato yalitokana  na haki za picha zake kwenye matangazo ya biashara.  Inakadiriwa alikwepa kulipa kodi ya takribani pauni milioni 12 (zaidi ya shilingi bilioni 58) kati ya mwaka 2011 na 2014 akiwa Real Madrid. 

Q BOY MSAFI - NAJUTA KUONDOKA LABEL WCB WASAFI

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi ya Diamond Platnumz amesema amesema kuwa anaomba msamaha kwa kuwa amemkosea Bosi wake ambaye ni Diamond Platnumz.  "Ni kweli nilikuwa namaanisha kuwa natamani nafasi niliyokuwa nayo WCB, Nikutokana na binadamu wapi nilipokosea nikizingatia kulikuwa na maneno mengi ya kutofautiana kwahiyo ni rasmi tu kuwaomba msamaha wale kabisa ambao mimi rasmi nimewakosea ili niweze kujiweka sawa," amesema Q Boy.  "Wanasema unapoonekana hauna tatizo na mtu ndani yako kuna kuwa na baraka pia, kwahiyo nimejifunza vitu vingi kupitia miaka hii miwili mitatu ambayo inaenda kwasababu kuna mambo yanaenda yanakuwa ni ya kitoto lakini kwa mtu anaeona mbali ni mtu ambaye nahitaji niwe sawa ili niweze kukamilisha kile ninachokifanya nisionekana nina tatizo na mtu yeyote ukianzia kiongozi wangu ambaye alikuwa ni Boss wangu Diamond, pia nimemtaka radhi Babu Tale , Mkubwa Fella pia na mama Diamond kama Famili," aliongeza Q Bo...

MWANAMKE ANAEDAI KUBAKWA NA CHRISS BROWN AFUNGUKA

Image
MSANII wa Marekani,  Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown,  anaandamwa na tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 huko Ufaransa usiku wa Januari 15 mwaka huu.  Mwanamke huyo amesema kwamba alifanyiwa tukio hilo baada ya kukutana na msanii huyo club huko ufaransa, na akamkaribisha chumbani kwenye hoteli aliyofikia iliyokuwa inajulikana kwa jina la ā€˜Mandarin Oriental Hotel.Mwanamke huyo amefunguka kwamba chumba walichotumia na Chris Brown ndipo alipomfanyia kitendo hicho  humo.  Chris Brown (Breezy) hajasema neno lolote juu ya taarifa hizo.  Taarifa zilizotolewa na chanzo cha Ufaransa cha  ā€˜Closer’,   kinaeleza kwamba Breezy yupo chini ya upelelezi wa polisi kuhusiana na tuhuma hizo.

MREMBO POSHY QUEEN AFUNGUKA KUHUSU SHEPU YAKE

Image
Mlimbwende maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini, Posh Queen, ameweka wazi chanzo cha kuwa na shepu ya kuvutia, baada ya tuhuma nyingi kuibuka kuwa ametumia dawa za kichina kuipata.  Akizungumza na www.eatv.tv, Posh amesema kwamba hivyo ndivyo alivyozaliwa na sio madawa, na kuhusu picha zinazomuonesha akiwa hana hiyo shepu, alikuwa mwembamba sana kiasi cha kushindwa kuonekana jinsi alivyoumbika.  ā€œZile picha zinaonesha nilikuwa mwembamba, sasa mtu mwembaba anakuwaje na shepu!?. Watu wanataka iwaje!?, mwisho wa siku ni mwili wangu,  sijatumia mchina au kitu chochote, lakini mtu anavyotaka kufikiri ni uamuzi wakeā€, amesema Posh.  Hivi karibuni zimezagaa picha za msichana huyo za zamani akionekana hana shepu, kitendo kilichowashangaza wengi ukilinganisha na muonekano wake wa sasa. 

OMMY DIMPOZ AIBUKA NCHINI KENYA ,TUTARAJIE KAZI MPYA

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ameonekana akiwa na msanii kutokana nchini Kenya, Will Paul Msafi kitu kilichoibua furaha kwa mashabiki wake.  Ommy Dimpoz amekuwa kimya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii toka Decemba Mosi mwaka jana. Kuliibuka taarifa za yeye kuzidiwa na kurishwa hospitali tena lakini taarifa hizo zilitupiliwa mbali na watu wake wa karibu.  Willy Paul amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika, 'Happy to see you my brother!! Ommy Dimpoz'  Ommy Dimpoz na Willy Paul amekutana Kenya, bado haijajulikana iwapo wawili hao wamekutana kwa lengo la kudumisha urafiki au ni kazi pekee. 

PAUL POGBA AKUBALI KUONGEZA MKATABA MAN UNITED

Image
Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba yupo tayari kuongeza kandarasi ya muda mrefu ndani ya Manchester United itakayomuwezesha kupokea kitita cha pauni 290,000 kwa wiki.  Mfaransa huyo aliyekuwa akilazimisha kutimkia Barcelona dirisha la usajili lililopita kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho sasa yupo tayari kusalia Old Trafford baada ya Mreno huyo kutimuliwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer.  Kwa mujibu wa The Sun, Pogba yupo tayari kusalia United chini Solskjaer huku akihitaji kuboreshwa kwa mkataba wake wa sasa ambao umesalia miaka miwili na nusu.  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa kwenye kiwango bora zaidi siku za hivi karibuni tangu kutua kwa meneja mpya Solskjaer huku akifanikiwa kufunga mabao matano na kuchangia pasi za mwisho zilizosaidia kupatikana magoli.   Kufuatia kutimuliwa kwa Mourinho mwezi Desemba, Pogba amejikuta akirudi kwenye kiwango ...

WACHEZAJI WATANO WA SIMBA WAONDOLEWA KWENYE MASHINDANO YA SPORTPESA CUP

Image
Mbelgiji Patrick Aussems ambaye ni Kocha wa Simba SC, amewaondoa wachezaji wake watano katika michuano ya SportPesa Cup inayoendelea hapa nchini huku jina la nahodha, John Bocco likiwa la kwanza.  Timu ya Simba inatarajiwa kuingia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuchuana na AFC Leopards katika michuano hiyo.  Aussems amesema wachezaji hao amewaondoa kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya majeruhi,  Mbelgiji huyo aliwataja wachezaji hao ni Bocco, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe wote wenye majeraha, Asante Kwasi matatizo ya kifamilia ambaye yupo kwao Ghana na Yusuph Mlipili yeye amemuweka kando kwa sababu ya kiufundi.  ā€œSheria za SportPesa zinaruhusu kuwatumia wachezaji 22 pekee, hivyo kama kocha tayari nimependekeza wanajeshi wangu nitakaowatumia katika michuano hii.  Hata hivyo amesema wachezaji wake wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji watano pekee ndiyo wanatarajiwa kuikosa michuano hiyo. 

MCHUNGAJI GWAJIMA ATOA USHAURI MZITO KWA RAIS MAGUFULI

Image
Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.  Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.  Kwenye ushauri huo Askofu Gwajima ambaye alianza kwa kumsifu Rais Magufuli, amesema kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye 'exposure' kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa. ā€œ Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure amba...

MCHEZAJI APOTEA KWENYE NDEGE BAADA YA KUSAJILIWA

Image
Mshambuliaji mpya wa klabua ya Cardiff City Emiliano Sala, amepotea angani kwenye ndege binafsi jana jumatatu jioni wakati anatoka mjini Nantes, Ufaransa kuelekea Cardiff, Wales.  Mamlaka ya anga ya Ufaransa imethibitisha ndege hiyo kupotea ambapo muargentina huyo mwenye miaka 28 alikuwepo pamoja na mtu mwingine wa pili.  Sala alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 18 siku ya Jumamosi na alikuwa ni miongoni mwa watu wawili waliokuwepo kwenye ndege hiyo iliyopotea.  Baada ya kusaini mkataba siku ya Jumamosi, Sala alirejea nchini Ufaransa kuwaaga wachezaji wa timu yake ya zamani ya Nantes, na baadaye kuweka picha akiwa na wachezaji hao katika Instagram akiandika ā€œ Kwa heri ya mwisho ā€œ kabla ya kupanda ndege kurejea Wales.  Afisa anayehusika katika kuitafuta ndege hiyo John Fitzgerald anasema kuwa hatarajii kumkuta mtu yoyote akiwa hai.  ā€œKuna bahati ya asilimia 5 tu ya kuwapata Sala na rubani, ā€œalisema Fitzgerald.ā€˜ Maji ni ya baridi sana k...

MATUNDA YANAYOWEZA KUBORESHA NGOZI YAKO

Image
Wakati mwingine ili uweze kuboresha mwonekanao wa ngozi yako si lazima utumie makemikali yenye viambatano vyenye sumu ili uweze kufanya hivyo, bali inahitajika uweze kutumia matunda ambayo yana msada mkuubwa wa kuweza kufanya ngozi yako ing`are.   1.   Parachichi.   Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juisi lakini huenda watu  hawalipendi kwa sababu kwa kutokuwa na sukari katika radha yake. Tunda hili lina vitamin kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini kwa wale walitumialo mara kwa mara, wanashauriwa kula au kunywa juisi ya parachichi wakati wowote endapo kama huna matatazo yeyote yananahusiana na kuzidi kwa mafauta mwilini. Pia tunda hili huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara.   2.   Apple.   Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupema umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamin na madini kibao, pia lina kazi sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngoz  y...

MAGAZETI YA LEO 19/01/2019

Image

MANCHESTER UNITED YAPATA PIGO KUBWA

Image
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, amethibitisha kuwa mchezaji wake Marouane Fellaini atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu au nne baada ya kuumia mazoezini.  Solskjaer pia amemzungumzia Scott McTominay kuwa ataendelea kusalia Old Trafford kwa kipindi hiki kilichobaki cha msimu huu, kwahiyo hatotolewa kwa mkopo kutokana na Fellaini kuwa majeruhi. Aidha Solskjaer amesema, Fellaini ataendelea kujituma ili kurudi kwenye mechi kubwa zijazo.

MAGAZETI YA LEO 16/01/2019

Image