RAIS MNANGAGWA AREJEA NCHINI ZIMBABWE KUTOKA KWENYE ZIARA
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.
Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.
Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic ChangeNelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.
Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitisha, Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo amekamatwa pia, Amesema vyombo vya ulinzi vimekuwa vikikamata familia za watu majumbani mwao.
Comments
Post a Comment