CRISTIANO RONALDO AKUBALI KULIPA FAINI YA BILIONI 50 BAADA YA KUKWEPA KULIPA KODI
Mchezaji wa Timu ya Juventus Cristiano Ronaldo amekubaliana na mamlaka za Hispania kulipa faini kuhusu kesi yake ya ukwepaji kodi.
Msemaji wa mahakama amethibitisha kwamba Ronaldo atalipa faini na kuepuka kifungo cha miaka miwili jela.
.
Hii inatokana na kwamba sheria za Hispania zinatoa nafasi kwa mtuhumiwa kuchagua adhabu ya jela au kulipa faini akipatikana na hatia ya kosa la kwanza.
Ronaldo atalipa takribani pauni milioni 17 zaidi ya shilingi bilion 49 za kitanzania alituhumiwa kukwepa kulipa kodi ya mapato yalitokana na haki za picha zake kwenye matangazo ya biashara.
Inakadiriwa alikwepa kulipa kodi ya takribani pauni milioni 12 (zaidi ya shilingi bilioni 58) kati ya mwaka 2011 na 2014 akiwa Real Madrid.
Comments
Post a Comment