Q BOY MSAFI - NAJUTA KUONDOKA LABEL WCB WASAFI


Msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi ya Diamond Platnumz amesema amesema kuwa anaomba msamaha kwa kuwa amemkosea Bosi wake ambaye ni Diamond Platnumz. 

"Ni kweli nilikuwa namaanisha kuwa natamani nafasi niliyokuwa nayo WCB, Nikutokana na binadamu wapi nilipokosea nikizingatia kulikuwa na maneno mengi ya kutofautiana kwahiyo ni rasmi tu kuwaomba msamaha wale kabisa ambao mimi rasmi nimewakosea ili niweze kujiweka sawa," amesema Q Boy. 

"Wanasema unapoonekana hauna tatizo na mtu ndani yako kuna kuwa na baraka pia, kwahiyo nimejifunza vitu vingi kupitia miaka hii miwili mitatu ambayo inaenda kwasababu kuna mambo yanaenda yanakuwa ni ya kitoto lakini kwa mtu anaeona mbali ni mtu ambaye nahitaji niwe sawa ili niweze kukamilisha kile ninachokifanya nisionekana nina tatizo na mtu yeyote ukianzia kiongozi wangu ambaye alikuwa ni Boss wangu Diamond, pia nimemtaka radhi Babu Tale , Mkubwa Fella pia na mama Diamond kama Famili," aliongeza Q Boy. 

Comments