AJALI YA BASI: Basi la kampuni ya Kisbo, linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dar-es-salaam kupitia barabara ya Itigi ambayo ipo kwenye matengenezo, limeanguka asubuhi majira ya saa mbili eneo la Kijiji cha Tura. Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinadai hakuna aliyepoteza maisha.