TAIRONE SANTOS WA SIMBA AANZA KUJIFUNZA KISWAHILI

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa beki mpya wa timu hiyo, Mbrazili, Tairone Santos Da Silva ameanza kujifunza Lugha ya Kiswahili na nyingine wanazotumia wachezaji wenzake. 

Hivi karibuni Aussems aliliambia gazeti hili kuwa Da Silva anasumbuliwa na tatizo la mawasiliano kwani hawezi kuzungumza na wachezaji wenzake kwa sababu hajui Kiswahili, Kingereza wala Kifaransa. 

Santos ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni anajua kuongea Lugha ya Kireno pekee ambayo mabeki wenzake wa kikosini humo hawaijui. 

Comments