OBREY CHIRWA ATUA MAKAO MAKUU YA YANGA
Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa, jana Alhamisi aliibukia Makao Makuu ya Klabu ya Yanga kwa ajili ya kushughulikia baadhi ya mambo yake na klabu hiyo.
Chirwa aliwahi kuitumikia Yanga kwa misimu miwili alipojiunga nayo msimu wa 2016/17 akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa timu hiyo.
Mshambuliaji huyo alitua klabuni hapo majira ya mchana ambapo alikutana na viongozi kadhaa wa Yanga na kujadili juu ya mambo yake, kabla ya kuondoka kwa kutumia usafiri wa gari aina ya Toyota IST.
Pamoja na kukutana na viongozi wa timu, pia straika huyo alikutana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambapo waliongea kwa muda ingawa haikufahamika walizungumza nini.
Chirwa ambaye msimu uliopita alifunga mabao 12 akiwa na Yanga, aliondoka ndani ya kikosi hicho na kutimkia Nogoom FC ya Misri, kisha akarejea Tanzania na kutua Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Comments
Post a Comment