KOCHA WA CHELSEA AWAACHA NYOTA 8 MCHEZO WA EUROPA
Kocha wa klabu ya Chelsea, Maurizio Sarri
ameamua kuwaacha wachezaji wake 8 kwa kuwapumzisha kuelekea mchezo wa Europa League dhidi ya klabu ya Vidi ya nchini Hungary.
Sarri amesema amechukua uamuzi huo baada ya kikosi chake kuwa kimecheza mechi nyingi mfululizo ndani ya mwezi huu na kwamba hii ndiyo nafasi sahihi ya kuwapumzisha nyota wake kwaajili ya michezo ijayo.
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo, Sarri amesema, "nimeamua kuwapumzisha wachezaji wote waliocheza mechi tatu mfululizo katika siku sita za wiki iliyopita kuelekea mchezo huu ".
"Wachezaji hao ni Kepa Arizabalaga, Cesar Azpilicueta,Ng'olo Kante na Eden Hazard. Pia tuna majeruhi, Matheo Covacic, Garrry Cahill na Victor Moses," ameongeza Sarri.
Pia kocha huyo amesema kuwa atautumia mchezo wa leo kwaajili ya kuwapa nafasi vijana wadogo wa timu hiyo akiwemo Callum Hudson-Odoi na Ethan Ampadu ambao wamekuwa wakifanya vizuri siku za hivi karibuni.
Chelsea inaongoza kundi lake la 'P' kwa jumla ya alama 15 mpaka sasa ikiwa imeshinda mechi zote tano. Inaingia katika mchezo huo ikiwa na uhakika wa kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo na kuongoza kundi hata kama itapoteza mchezo wa leo.
Comments
Post a Comment