VANESSA MDEE AFUNGUKA KUACHA NA JUX
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee 'Vee Money' amefunguka juu ya madai yanayosambaa mitandaoni kuwa amemwagana na mpenzi wake, Juma Jux.
Vanessa ambaye yupo nje ya nchi kikazi amesema kuwa, hajamwagana na mpenzi wake huyo bali ni masuala ya kazi tu ndio yamewaweka mbali na kwamba hakuna kingine zaidi ya hicho.
Akizungumzia madai ya kuwa amemsaliti, Vanessa amesema kuwa hana tatizo kabisa na Jux ila kazi ndiyo zinazowafanya wasiwe karibu hivyo ndiyo maana watu wanawaona kama hawapo sawa.
“Mimi na Jux hatuwezi kuwa pamoja kila siku kuna kipindi kazi zinabana sana na ndio maana watu wanaona tumemwagana, niwatoe hofu tu mashabiki zangu kwamba tupo sawa na hakuna kitu chochote kibaya”, amesema Vanessa.
Www.eatv.tv, imemtafuta Juma Jux ili kuzungumzia tuhuma hizo zilizoenea mitandaoni kuhusu kusalitiwa na mpenzi wake huyo lakini simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa.
Comments
Post a Comment