THERESSA MAY ANUSURIKA KUTOLEWA MADARAKANI NA CHAMA CHAKE
Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May amepata ushindi baada ya wanachama wa chama cha Conservative kupiga kura ya kutokuwa na imani na uongozi wake.
May ameungwa mkono na wabunge 200 katika kura hiyo huku wengine 117 wakiwa wamepiga kutokuwa na imani naye.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza atanusurika kupigiwa tena kura kama hiyo mpaka baada ya mwaka mmoja.
Chama cha upinzani kinaweza kuamua kupiga kura dhidi ya uongozi wa serikali ya May lakini wanachama wameamua kuwa huu sio muda mwafaka.
"Matokeo ya kura ya leo yameonyesha kuwa wabunge hawana imani",alisema mwenyekiti wa kamati ya 1922,uongozi wa chama cha Conservative.
Brandy alipokea barua 48 za kutaka kura ya kutokuwa na imani ipigwe.
Hata hivyo waziri May amesema kuwa hana haja na kugombea katika uchaguzi mwaka 2022 na kwamba dhumuni lake kuu ni kuhakikisha anamalizana na suala zima la Brexit.
Comments
Post a Comment