Posts

Showing posts from September, 2019

Simba yaiadhibu kagera sugar ya bukoba 3-0

Image
Timu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.   Mshambuliaji wa Simba , Medie Kagere ndiye alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Kagera Sugar kunako dakika ya 5 ya mchezo na dakika ya 79 akafunga la pili kwa mkwaju wa penalti, goli la pili la Simba lilifungwa na Mohamed Hussein dakika ya 35.  

Rais Magufuli amteua rais mstaafu Mwinyi kua mkuu wa chuo MUHAS

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kuwa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).   Mhe. Mwinyi ameteuliwa kuendelea na wadhifa huo kuanzia leo September 25, 2019.

Lionel Messi ashinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA 2019

Image
Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo lilihitimisha kilele cha utoaji wa tuzo za FIFA The Best 2019 kwa kutangaza wachezaji mbalimbali waliofanikiwa kushinda.   Tuzo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ni tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiume ambapo ilikuwa ikiwaniwa na Virgil van Dijk wa Liverpool, Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa FC Barcelona.   Ronaldo hakutokea katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika Italia na Lionel Messi kuibuka mshindi kwa mwaka 2019 na kuwashinda Ronaldo na Van Dijk, hii ndio mara ya kwanza kwa Messi kushinda tuzo hiyo toka mfumo mpya uanzishwe.   Jurgen Klopp wa Liverpool akiibuka kocha bora wa mwaka, Megan Rapinoe raia wa Marekani akiibuka mchezaji bora wa mwaka wa kike

Rekodi za Zlatan Ibrahimovic baada kufikisha miaka 30

Image
Zlatan ibrahimovic baada ya kufikisha miaka 30  na kuondoka katika klabu ya manchester united, kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini marekani kunako klabu ya LA Galaxy. Baada ya miaka 30 hizi ndizo rekodi alizoweka zlatan ibrahimovic "super ibra"

Golikipa wa chelsea amshambulia vikali De gea

Image
Kipa wa zamani wa Chelsea,  Mark Schwarzer, amesema kuwa mlinda mlango namba moja wa Manchester United, David de Gea amekuwa akionyesha uwezo wa kawaida tofauti na zamani.   Schwarzer amesema kuwa mabao mengi anayofungwa yanatokana na makosa yake binafsi.   ā€œMabao mengi anayofungwa yametokana na makosa yake binafsi, makosa aliyofanya kipindi hicho ni mengi kuliko aliyofanya miaka sita au saba, iliyopita,ā€ alisema Schwarzer .   Schwarzer amesema De Gea alikubali kufungwa kwa uzembe kwenye michezo ya Ligi Kuu England wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace na Southampton.   De Gea ambaye amesaini mkataba mpya ndani ya United utakaodumu mpaka 2023, amekuwa akibebeshwa lawama kwa kufanya makosa yanayopelekea timu yake kufungwa.   Hivi karibuni mlinda mlango huyo mashuhuri wa mashetani wekundu alisaini mkataba mpya ambao unamuwezesha kubaki Old Trafford hadi mwaka 2023 huku akilipwa mshahara wa Paundi 500,000 kwa juma.

Mrembo Hamisa Mobetto atamani maisha ya ndoa

Image
Hamisa Mobeto siku za nyuma aliwahi kusema Hana mpango wa kuolewa na kijana wa kitanzania Bali mipango yake ni kuolewa na mzungu   Awali alisema yeye anataka labda mwanaume mzungu au mtu mzima, awe alishawahi kuachwa au mgane kwa hiyo ndio hivyo, na kusema kijana kwake hapana.   Hamisa Anataka mtu wa kumuoa awe angalau miaka 45 kwa sababu yeye mwenyewe ana watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wake

Golikipa ya Bayern munich Manuel Neur atangaza kustaafu soka baad ya msimu ujao

Image
Golikipa wa Bayern Munich Manuel Neur(33) amesema anafikiria kustaafu soka la ushindani ya kumalizika kwa msimu ujao. Manuel Neur ambaye ameitumikia Bayen Munich na timu ya taifa ya ujerumani kwa mafanikio makubwa anaamini muda huo utakua muda muafaka kwake kuachana kabisa na masuala ya soka la kulipwa.

Matokeo ya mechi zote za UEFA hatua ya makundi

Image
Mechi za michuano ya UEFA champions league hatua ya makundi zimemalizika na tumeshuhudia Mbwana samatta amabae ni  mtanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo akifunga goli akiwa na timu yake ya Genk. Yafuatayo ni matokeo ya mechi zote za michuano hiyo kwa hatua ya makundi

Mbwana Samatta mtanzania wa kwanza kucheza na kufunga goli UEFA

Image
Ni historia mbili mpya Mbwana Samatta ameandika usiku uliopita. Amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano ya Klabu bingwa Ulaya na pia wa kwanza kufunga goli kwenye michuano hiyo.   Hata hivyo, furaha yake ya kuweka rekodi binafsi imegubikwa na matokeo mabaya baada ya klabu yake ya KRC Genk kupokea kipigo kizito cha goli 6-2 kutoka kwa RB Salzburg.   Samatta alipachika bao lake wavuni katika dakika ya 52, lakini halikuweza kubadili mwelekeo wa mchezo sababu mpaka muda huo walikuwa nyuma kwa goli 5-1.   Awali kulikuwa na hofu juu ya afya ya Samatta na iwapo angecheza mechi hiyo baada ya kuumia goti alipokuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi Hivi Karibuni.   Hata hivyo majeraha hayo madogo yalipona kabla ya mchezo wa jana usiku ambapo alicheza kwa dakika 85.   Mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Genk alikuwa mshambuliaji Erling Braut HĆ„land aliyepachika magoli matatu katika dakika ya dakika ya 2',34' na 45'.   Katika mchez...

Cristiano Ronaldo amlilia baba yake mzazi

Image
Ronaldo, amwaga machozi baada ya kuulizwa sawali kuhusu baba yake, Alipoulizwa jinsi alivyokuwa akijisikia baada ya  kusikia baba yake akiongea juu ya kiburi chake kwa mafanikio ya mwanawe, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliongezea:   ā€œNdio.ā€Nadhani mahojiano yangekuwa ya kuchekesha, lakini sikutarajia kama ntalia kulia. Lakini sikuwahi kuona picha hizi wala ā€œSijawahi kuona video yeyote kitu ambacho hakiwezekaniā€ Sijui iko wapi … Lazima niwe na picha hizo kuonyesha familia yangu. ā€œLakini sikumjua baba yangu asilimia 100. Alikuwa mtu mlevi sana. Sikuwahi kuongea naye, kama mazungumzo ya kawaida. Ilikuwa ngumu sana ā€   Ronaldo aliongeza kuwa ā€œFamilia yangu imeona mafanikio yangu, mama yangu ameyaona, Ndugu zangu pia, hata mtoto wangu wa kwanza pia, lakini baba yangu, hakuona chochote, pia hakuona wakati nashinda tuzo na ilitakiwa ayaone… alikufa angali mdogo. ā€

Kikosi cha Taifa stars kinachoshiriki michuano ya CHAN

Image
Hiki hapa kikosi cha wachezaji 25 waliochaguliwa kushiriki michuano ya CHAN kwenye mchezo dhidi ya Sudan

Hamza Bin laden mtoto wa Osama auawa na jeshi la marekani

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliuawa katika operesheni ya Marekani.   Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.   Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita. Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.   Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.   ''Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan / Pakistan''.Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu ya Whitehouse.  

Azam Fc yachezea kichapo kombe la mabingwa Afrika

Image
Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United wamepoteza kwa kukubali kufungwa goli 1 kwa bila.   Bao pekee la Triangel United ya Zimbabwe lilifungwa dakika ya 34 na Ralph Kawondera kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa Azam FC.   Licha ya Azam FC kupewa sapoti kubwa na mashabiki waliojitokeza uwanja wa Azam Complex hayakuzaa matunda kwani safu ya ulinzi ya Triangle United ilikuwa ngumu na ikajilinda na hatari zote.   Sasa Azam FC ina kazi nzito ya kwenda kutafuta matokeo ugenini kwenye mchezo wa marudiano unaoatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27-29 nchini Zimbabwe.

Rayvanny kumzima Harmonize baada ya kuondoka WCB

Image
TANGU kuondoka kwa mwanamuziki Rajab Abdul ā€˜Harmonize’ kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) kuna harakati za ndani zinazofanywa kumpaisha memba mwingine wa kundi hilo, Raymond Mwakyusa ā€˜R ayvanny’.   Habari za chini ya kapeti zilieleza kuwa, mwaka huu wa 2019 huenda ukamalizika kwa mafanikio makubwa kwa Rayvanny kutokana na ā€˜fujo’ zinazofanyika za kumpaisha kimataifa.   Ilielezwa kuwa, kasi yake ya kufanya kolabo za kimataifa ni kubwa kama aliyokuwa nayo Harmonize au Harmo alipokuwa ndani ya lebo hiyo.   Mpaka sasa Rayvanny ameshafanya kolabo na wanamuziki wakubwa duniani kama Pitbull, Jason Derulo na Nora Fatehi.   Habari nyingine nzito ni kwamba kwa sasa Rayvanny yupo kwenye maandalizi ya kolabo na mwanamuziki aliyewahi kufanya kazi chini ya lebo ya rapa mkubwa duniani, Jay-Z kupitia lebo yake ya Roc Nation anayefahamika kwa jina la Philly Freeway.   Kwa mujibu wa prodyuza maarufu wa Bongo Fleva, S2kizzy, Rayvanny na jamaa huyo tayari wameingia studio...

Jurgen Klopp achaguliwa kocha bora wa mwezi na Pukki mchezaji bora

Image
Meneja wa klabu ya liverpool ya jijini London ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa nane baada ya kuwapiga chini makocha wa Totenham,Manchester united na Manchester city, Timu ya liverpool imecheza michezo minne na kushinda mechi zote 4. Upande mwingine mshambuliaji wa klabu ya Norwich city Teemu pukki ameahindi tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nane baada ya kucheza mechi  4 na kufanikiwa kufunga magoli 5 katika michezo hiyo.

Kikosi cha Simba leo dhidi ya Mtibwa sugar

Image
Klabu ya Simba imetoa kikosi kitakachocheza leo dhidi Mtibwa sugar, kikosi hicho kina wachezaji 11 na 7 wa akibaki kikiwa kinaongozwa na Nahodha  Mohammed hussein, Mchezo huo utachezwa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Ben pol apigia msumari ndoa yake na Anerlisa

Image
Baada ya uvumi wa maneno ya waja kuhusu mastaa kuchumbia au kuchumbiwa na kuacha au kuachwa solemba, mwanamuziki wa RnB Bongo, Benard Paul ā€˜Ben Pol’ amevunja ukimya.  Baada ya kumchumbia mrembo tajiri kutoka nchini Kenya, Anerlisa Muigai, wengi walitarajia kuwa kilichokuwa kinafuata ni ndoa kati ya Ben Pol na mrembo huyo, lakini miezi ikawa inakatika tu huku baadhi ya wananzengo wakidai uchumba huo umevunjika.   Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, mapema wiki hii, Ben Pol alieleza kuwa mipango ya ndoa iko palepale. Alisema suala hilo ni la kifamilia zaidi hivyo mashabiki wake wasisikilize maneno ya watu, bali wasubiri waone nini kitakachofuata.   ā€œUnajua kuna kitu watu wanachanganya, mambo ya ndoa ni ya familia zaidi, siyo kila kitu unatakiwa kukiweka wazi. ā€œKwa hiyo, watu watulie ili waone nini kitatokea na kama ikitokea, muda ukifika wataona tu kwa sababu ndoa siyo jambo la siri na lazima kabla ya hapo watu watapata taarifa tu.   ā€œKwa sas...

Amber lulu amkana Ommy dimpoz mchana kweupe

Image
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu, ametaja list ya wasanii ambao amadai hawezi kutoka nao kimapenzi kwa namna yeyote ile.   Katika orodha hiyo Amber Lulu amemtaja msanii wa kwanza ambaye hawezi kutoka naye ni Dudubaya, Ommy Dimpoz, Alikiba na wengine wengi.   Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia kurasa za Facebook na YouTube za East Africa Television, Amber Lulu amesema, "siwezi kutembea na msanii kama Dudubaya anaongea sana, Kalapina yeye ni mkorofi sana, Ommy Dimpoz yeye hana habari na wanawake sijui kwanini".   Kwa sasa Amber Lulu anatamba na ngoma ya 'Haters' ambayo anatarajia kutoa video wiki ijayo

Msanii P didy atarajia mtoto na mrembo Lori harvey

Image
BAADA ya kuibuka tetesi kisha ikawa kweli, hatimaye mkongwe katika gemu la Hip Hop kutoka Marekani, P Diddy (49) anatarajia kupata mtoto kwa mrembo, Lori Harvey (22).  Ishu ya mkongwe huyo kutarajia kupata mtoto imekuja siku chache baada ya wawili hao kunaswa mapumzikoni huko Cabo, Mexico   Katika picha mbalimbali zilizosambaa mitandaoni, zinamuonesha Lori akiwa ameshika tumbo lake kama vile anaonesha ujauzito na nyingine zikimuonesha P Diddy akiwa amelishika tumbo la Lori.   Mwezi uliopita P Diddy aliungana na familia ya Lori pamoja na kukutana na wazazi wake wakati wapo mapumziko nchini Italia

Kim kardashian aingiza zaidi ya billioni 4 ndani ya dakika 8

Image
Utajiri wa Familia isiyoishiwa na vituko ya The Kardashian sio tu Mamilioni ya watu ambao wanawafatilia kila mahala bali ni ushawishi walionao kwa hao watu, Inaripotiwa Kuwa Kim Kardashian Siku ya Jana (Sept. 10) ameingiza zaidi ya Tsh. Billion 4.5 ( $ 2M) Ndani ya dakika chache tu baada ya bidhaa zake mpya za nguo (SKIMS) kuanza kuuzwa.   Bidhaa hizo mpya ndani ya siku moja tayari zimetajwa kuwa tishio kwa makampuni makubwa ya nguo za ndani za wanawake, Kampuni maarufu ya Spanx ilipata faida ya Dola Million 4 Mwaka wao wa Kwanza Lakini Kim K Tayari ameshaitengeneza nusu ya hizo Pesa ndani ya Dakika Tu. Hata Hivyo haishangazi sana ukiangalia na idadi ya watu wanaomfata kwenye Mitandao ya Kijamii, Kim K ana idadi ya Follower Million 147 Kwenye Instagram na Million 61.5 Kwenye Mtandao wa Twitter.   TMZ wameripoti kuwa kabla ya #KimKardashian kuziachia rasmi hizo bidhaa za nguo za wanawake alilazimika kusogeza mbele hadi siku ya Jumanne (Septemba 10) kutokana na Mtandao ulio...

Shabiki wa Yanga atembea kwa miguu hadi zambia kuangalia mpira

Image
Mwanachama na shabiki wa klabu ya Yanga leo ameanza safari ya kutembea kwa mguu kutoka Iringa kwenda Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kati ya Zesco United na Yanga mchezo ambao utachezwa September 26 katika dimba la Levvis Mwanawasa Stadium  

Mbwana samatta aendelea kuuguza majeraha ya goti

Image
Nahodha wa Taifa Stars, Mshambuliaji Mbwana Samatta, Jumapili alipata majeraha ya goti kwenye mechi dhidi ya Burundi na kumlazimu kocha kufanya mabadiliko dakika ya 106 akiingia Himid Mao.   Mara baada ya kumalizika kwa mchezo alikwea pipa (Jumatatu) na kurejea Ubelgiji katika klabu yake ya Genk.   Baada ya kufika Ubelgiji, Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram Samatta ameeleza kuwa tayari amefanyiwa vipimo vya MRI katika goti.

Timu bora za UEFA mwaka 2019 Madrid yaongoza

Image
UEFA wametoa list ya timu bora za mpira wa miguu duniani kwa mwaka 2019. klabu ya Real madrid ikiwa imeshika  nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Atletico Madrid nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na Barcelona zote za nchini uhispania. Huku upande mwingine timu za uingereza zimeongozwa na Manchester city iliyoshika nafasi ya 6 na Liverpool nafasi ya 8. Angalia picha inayofuata hapa chini kujua timu zote zilizoingia kwenye list ya uefa mwaka huu

Yanga yatangaza kamati mpya ya hamasa mbotto na uwoya ndani

Image
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ameteua Kamati ya Kudumu ya Hamasa yenye wajumbe 21 ikiongozwa na Suma Mwaitenda katibu wake akiwa Deo Mutta.   Baadhi ya wajumbe walioteuliwa kuingia kwenye kamati hiyo ni Irene Uwoya, Jaquiline Wolper, Miriam Odemba, Flora Mvungi, Haji Mboto, Dominick Salamba, Hassan Bumbuli, Khamis Dacota, Jimmy Msindo na Jimmy Mafufu

Meneja wa Harmonize afunguka kuhusu ndoa ya Hamonize na Sarah

Image
Meneja wa msanii Harmonize, Beauty Mmari almaarufu kama Mjerumani, amepinga kuwa nyota huyo alifunga ndoa na mpenziwe Sarah Michelloti mnamo Ijumaa, Septemba 7 Picha za staa huyo wa wimbo maarufu wa 'Kadamshi' na mchumba wake aliyekuwa amevalia gauni lililoashiria wawili hao walikuwa wanafunga ndoa zilisambaa mitandaoni huku maelfu ya mashabiki zake wakimpongeza.    Kwa mujibu wa Nyakati.com, baadhi ya wafuasi wao mitandaoni walishangaa ni vipi nyota huyo alifanya harusi kisiri pasi na hata kuwaalika wasanii tajika kutoka Tanzania. Hata hivyo, meneja wa Harmonize, Mjerumani amepinga kwamba wawili hao walifunga ndoa na kusema kwamba Sarah alikuwa akiigiza katika wimbo ambao staa huyo anatarajia kuutoa hivi karibuni     "Harmonize hakufunga ndoa Jumamosi iliyopita, ila alimshirikisha mpenziwe kwenye video ya wimbo wake atakaoutoa hivi karibuni wa 'Marry Me'. Wazo nzima la wimbo huo ni sawia na lile Diamond alitumia na kumshirikisha Zari katika wimbo wake wa ...